Header Ads


BAADHI YA WANANCHI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA KATAVI WAMELALAMIKIA KITENDO KILICHOFANYWA NA MADAKTARI BINGWA


Wakazi wa mpanda wakiwa katika uwanja wa polisi katika manspaa ya mpanda


MPANDA-KATAVI
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo  mbalimbali ya mkoa  wa  Katavi wamelalamikia kitendo kilichofanywa na  Madaktari bingwa cha kusitisha ghafla na bila taarifa huduma ya upimaji na utoaji wa  matibabu ya  magonjwa yasiyo ambukiza nakisha kuondoka nakuwaacha bila kuwahudumia. 

Madaktari hao wa  magonjwa  mbalimbali  yasiyo  ambukiza wa kutoka tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na hospital ya Oceanroad walikuwa wakitoa huduma katika uwanja wa Polisi uliko  Manispaa ya Mpanda mkoani humo. 

Huduma za upimaji  wana utoaji wa matibabu ya  magonjwa  yasiyoambukizwa ulizinduliwa  juma  tano  ya  wiki  iliyopita  na  waziri wa  afya Maendeleo  ya  Jamii Jinsia Wazee na  watoto  Ummy  Mwalimu.

Madakitari  hao walikuwa  wameletwa  Mkoani Katavi  kwa  ajiri ya  kutoa  huduma  hizo na Mbunge wa  Viti  Maalumu mkoani humo Anna  Lupembe  ambae  alipita  katika  Wilaya  zote  tatu  za mkoa huo na  kuwatangazia  wananchi  na  kuwahakikishia  kuwa huduma  za madaktari  hao  zitakuwepo  hadi  siku ya ijumaa  lakini  zilisitishwa  siku moja kabla na  kuwasababishia wananchi hasara  za  gharama  kwa  wananchi waliokuwa wametoka  vijijini.

Mkaziwa  Kijiji  cha  Karema  Said  Juma  alisema  yeye  ni  mmoja  wa   wakazi  wa  Tarafa ya Karema  aliyesafiri  umbali  wa  kilometa  130 kwa  ajiri kufuata huduma zinazotolewa na madaktari  hao  lakini  alipofika  kwenye  eneo  waliokuwa wakitolea  huduma alikuta   mabanda  yako  wazi   huku kukiwa  hakuna  daktari  bingwa  hata  moja nawagonjwa wamekaa.

Naye Abel  Kalifumu   Mkazi   wa  Tarafa ya  Inyonga  Wilayani  Mlele  alieleza  kuwa yeye  na  wenzake  walifika   Wilayani  Mpanda kwa   ajiri ya  kupatiwa  huduma  baada ya Mbunge    Lupembe  kuwatangazia  kwenye  mkutano wa  hadhara  uliofanyika  siku ya alhamisi   katika   viwanja  vya  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Mlele  kuwa  huduma  itakuwepo  mpaka siku  ya  ijumaa na wakasafiri kesho yake alfajiri  lakini  walipofika mjini   Mpanda walikuta hakuna  huduma.

Hata hivyo taarifa  za  kutoka  ndani ya  vyanzo  vya   habari  vinadai kuwa kulikuwa  na  kutofautiana kwa  baadhi ya  makubaliano  baina  ya  madaktari bingwa  na  mwenyeji  wao  ambaye ni mbunge Lupembe hali iliyopelekea hata mafuta ya gari aina ya basi walilokuwa wakilitumia madaktari hao lilitakiwa kuwekwa mafuta na mbunge huyo wakati wa kuwarudisha  Dar es  salaam lakini ilibidi yatolewe na  Ofisi  ya Mganga  Mkuu wa  Mkoa huo kutokana na tofauti iliyojitokeza. 

No comments

Powered by Blogger.