WANANCHI WA KIJIJI CHA SHOMOLA KATA YA MLANGALI WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMEUPONGEZA UONGOZI WAO
Wakazi wa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe |
MBOZI-SONGWE
Wananchi wa kijiji cha shomola kata ya mlangali wilayani
mbozi mkoani songwe wameupongeza uongozi wao kwa kuwahamasisha katika shughuli
mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya
msingi shomola
Wakizungumza na blog hii wananchi hao JULIUSI MWASANGA pomoja na RENA
MWAJAJA wamesema kuwa uongozi wa kijiji
unawahamasisha mara kwa mara shughuli mbalimbali za maendeleo na kwa sasa wameshaanza ujenzi
wa nyumba nne za walimu ambazo zinatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 mwezi
wa nane mwaka huu.
Kwaupande wao walimu wa shule hiyo ya shomola
akiwemo BONIVENTURE MGALLA wamesema kuwa wanashilikiana vema na wananchi pamoja
na viongozi katika ujenzi wa nyumba hizo na kuendelea kuushukuru uongozi kwa juhudi za uhamasishaji wa maendeleo ndani
ya kijiji hicho.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji hicho
SHADRACK MGALLA amesema kuwa ujenzi huo
unategemea nguvu kubwa kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakijitoa
katika shughuli hizo za ujenzi wa nyumba za walimu kwa kutoa michango na
kuwataka wananchi kuendelea kujitoa vivyo hivyo katika shughuli hizo.
Pia MGALLA ameendelea kwa kuongeza kuwa wananchi
waendelee kujitoa kufanya maendeleo bila ya kutegemea misaada kwakua misada
inaweza kuchelewa na kwa wale watakao kaidi kuhudhuria katika shughuli hizo za
maendeleo watachukuliwa hatua za kisheria.
Post a Comment