JAMII YA WATU WA MKOA WA RUKWA WASHAURIWA KUTO KUWARAUMU WATOTO WAO PINDI MAENDELEO YAO YA KIELIMU YANAPOKUWA MABAYA.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Julius Mseleche Kaondo |
NKASI-RUKWA
JAMII mkoani Rukwa imeshauriwa
kubadilika kifikra na kuacha tabia yak kuwalaumu watoto pindi maendeleo yao ya
kielimu yanapokuwa sio mazuri badala yake wajenge tabia ya kuwapima watoto wao
uwezo wa afya ya mwili ili wajue wanaweza kupewa elimu Katika mfumo gani.
Hayo yalibainishwa jana na
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo Julius Kaondo wakati
akizindua kituo maalumu cha upimaji wa kielimu (Nkomolo Assessment Centre)
Kilichopo Katika eneo la shule ya msingi Nkomolo wilayani humo.
Alisema kuwa wapo baadhi ya wazazi
ambao wamekuwa na tabia ya kuwalaumu watoto wao kutofanya vizuri shuleni lakini
hawajishughurishi kuwapima ili kutambua uwezo wao tangu wakiwa wadogo.
Kaondo alisema kuwa ifike wakati
wazazi wakawathamini watoto wao kwakuwapima viungo vya mwili kama macho,
masikio pamoja na afya ya akili pi vipimo vingine ambavyo vitasaidia kutambua
changamoto alizonazo mtoto na pia itakuwa rahisi kumuhudumia.
Alisema kuwa kituo hicho kitakuwa
kikitoa huduma kwawakazi wa mikoa ya Rukwa na Katavi hivyo nivizuri kitumike
kuwapima watoto na watu wazima ili waweze kupewa huduma stahiki kutokana na
tatizo litakalobainika.
Awali akizungumza kabla ya kuzindua
mradi huo mkurugenzi wa maradi huo unaojulikana kama international aid service
( ias) Irene Shayo alisema kuwa maradi huo unafadhiliwa na nchi ya Denimark
wakishirikiana na kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT).
Alisema kuwa mpaka hivi sasa kituo
kikubwa ni kilichopo wilayani Nkasi ambacho kitatoa majibu ya changamoto nyingi
zinazowakabili wakazi wa mikoa hiyo miwili na aliwasisitiza kukitumia
iliwanufaike na uwepo wakituo hicho.
Shayo alisema kuwa lengo ni kuongeza
fursa anuai kwa watoto na watu wazima wanaotengwa Katika jamii iliwaweze
kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo ambazo zimekuwa zikiwapita kutokana na kutengwa
kufuatia changamoto walizonazo.
Post a Comment