MSUVA SAFARI YAIVA MOROCCO
"Kila kitu kipo tayari nasubiria viza tu itoke, Ntaelekea Morroco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida (washindi wa pili ligi kuu Morroco). . Naondoka Yanga SC , timu iliyonilea na kunipa mafanikio . . Siondoki kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, naamini ipo siku ntarudi kuitumikia Yanga tena ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini, baada ya Morroco mungu akijalia basi itakuwa Ureno lakini hasa hasa ni Spain maana nna uwezo wa kucheza La Liga . . Ahsante wana Yanga kwa ushirikiano mlionipa naamini kupitia kipaji changu kuna furaha nimewapa"
- SAIMON MSUVA.
Post a Comment