WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF,JUMANNE MAGHEMBE AMEWATAKA WANANCHI KUACHANA NA MAWAZO KUWA IPO SIKU SERIKALI ITAKATA ENEO LA HIFADHI NA KUWAPATIA WANANCHI
NKASI-RUKWA
.Hayo ameyasema jana
alipozungumza na Wananchi wa vijiji vya lyazumbi na Kizi wilayani Nkasi mkoani
Rukwa baada ya Wananchi wa maeneo hayo kumuomba waziri awamegee sehemu ya ardhi
iliyopo katika hifadhi ya Lwafi kwa ajiri ya kuendeshea shughuli mbalimbali za
kiuchumi..
Alisema Tanzania bado ina sehemu
kubwa ya watu kuendelea kufanyia shughuli zao bali kilichokosekana ni
kutokuwepo kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
kauli hiyo aliitoa baada ya mmoja wa
wananchi katika kijichi cha Lyazumbi Hamisi Kiswaga kumuomba Waziri awamegee
sehemu ya ardhi iliyopo ndani ya hifadhi akipatie kijiji hicho kwa lengo la
kupanua kijiji na kupata eneo kubwa la ardhi kwa ajiri ya kufanyia shghuli zao
za kiuchumi
Sambamba na hilo Waziri Maghembe
ameiagiza serikali wilayani Nkasi kuhakikisha kuwa wanatengeneza kisima cha
maji haraka katika kijiji cha Lyazumbi ili wakazi wa kijiji hicho
waweze kupata maji ya kutosha ili waache kuingia ndani ya hifadhi kutafuta maji
kama ilivyo sasa kitu ambacho ni hatari sana.
alisema kuwa hivi sasa wakazi wa
kijiji hicho wanategemea maji kutoka ndani ya hifadhi baada ya bomba lao
kuharibika na kuwa kitu hicho hakikubaliki bali serikali sasa ya wilaya
itengeneze haraka bomba la kisima katika kijiji hicho ili watu wasiingie tena
ndani ya hifadhi kusaka maji.
"Ni kosa kubwa watu kutegemea
huduma ndani ya hifadhi maana wanaweza kukumbana na majanga mbalimbali ndani ya
hifadhi na sheria hairuhusu jambo hilo hivyo wilaya tengenezeni kisima hicho
haraka ili kusiwepo mwingiliano kati ya hifadhi na mahitaji ya
watu"alisema Maghembe
Awali mkuu wa wilaya alimuomba
waziri Maghembe asiwaamishe wakazi wa kijiji cha Kizi kwa kuwandoa chini ya
sheria ya mita 500 kutoka hifadhini na kuiomba serikali iutambue mpaka kati ya
hifadhi na kijiji iwe ni barabara ya lami kitu ambachoi waziri amekikubali
Post a Comment