WILAYA YA MOMBA MKOANI SONGWE YAZIDI KUSHAMBULIWA NA UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO NA KIPINDUPINDU
MOMBA-SONGWE
ASILIMIA 80% ya wananchi wa vijiji
vya Chole na Mkomba kata ya Mkomba wilaya ya Momba mkoani Songwe wanaugua homa
za matumbo ikiwemo kipindupindu na kuhara kutokana na tatizo la kukosekana kwa
maji safi na salama ambapo wamesema wanalazimika kutumia maji machafu yasiyo
salama ambayo hata hivyo hayapatikaniki kirahisi hivyo kuitaka serikali katika
bajeti yake ya mwaka 2017/2018 itoe kipaumbele vijijini katika kutatua
kero ya maji.
Wananchi hao
wamekiambia kituo hiki kuwa tatizo
hilo ni la muda mrefu , na
kuwa kutokana na hali hiyo
wamekuwa wakipata magonjwa ya milipuko
na kuomba serikali kuwangalia kwa
jicho la tatu ili kuweza kuondokana
na adha hiyo kama wananvyo
bainisha zaidi menance maarifa makazi wa
mkomba na ernesti sichimbo makazi wa chole.
Hali hiyo imefanya
Mwenyekiti wa kijiji cha Chole Damian Sichila na Diwani wa kata ya Mkomba
Colletha Mwanselela kupaza sauti zao na
kusema katika vitongoji 25 ni kitongoji kimoja tu chenye unafuu wa
maji huku vingine 24 havina maji na kuongeza kuwa katika bajeti ya mwaka
2016/2017 kata ya Mkomba ilitengewa fedha za maji million 16 lakini
hazikutolewa mpaka hivi sasa , hivyo kuiomba halmashauri
kuhakikisha bejeti ya mwaka huu inatekelezeka.
Vongozi wa halamashauri ya wilaya ya Momba
akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Juma said Irando ,
maua mgalla kaimu mkurungezi na matha
chikoti mwenyekiti wa halamashauri ya
momba , ambao licha ya kukiri kuwepo kwa kero hiyo wamesisitiza
kuwa fedha zilizotengwa na serikali kuu kwa ajili ya maji, vijiji vyenye
kero kubwa zaidi kikiwemo cha Chole vimepewa kipaumbele.
Post a Comment