AFISA MTENDAJI RUNGWE AKUTANA NA MKONO WA TAKUKURU
RUNGWE-MBEYA
AFISA mtendaji wa kata ya Simike
wilayani Rungwe mkoani Mbeya,Rehema Maraso amejikuta akiwa mikononi mwa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kuhojiwa kwa saa kadhaa baada ya
kutuhumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo kutoza fedha
pasipo kutoa risiti.
Akizungumza jana na gazeti
hili,mkazi wa kijiji cha Kagwina Award Kalonga,alisema mtendaji huyo amekuwa
akitumia vibaya madaraka yake kwa kuwatoza watu ushuru pasipo kuwapa lisiti na
kuwa mbali na mambo mengine alimtoza faini mkazi wa kijiji cha Kalalo
Richard Gwakabale,pasipo kumpa lisiti na kujikuta akiwa mikononi mwa Takukuru.
Mkazi wa kijiji cha Kalalo Richard
Gwakabale,alisema ilikuwa tarehe 14 Augost 2017 aliitwa ofisi ya kijiji ambapo
mtendaji aalimueleza alipe faini kwa kusababisha kutofikia lengo la makusanyo
kwa sababu ya kuwahamasisha wafanyabiashara kutolipa ushuru,licha yan kuwa
serikali imekataza ushuru kwa wakulima wadogo.
Alisema baada ya hapo aliambiwa na
afisa mtendaji wa kijiji cha kalalo,aliyafahamika kwa jina la Murid kuwa
kijiji kimeweka malengo ya makusanyo ya, ushuru kwa siku 50,000 na kwakuwa
hawajafia lengo na kutakiwa kulipa faini Tsh, 50,000 ambazo amezilipa na baada
ya kulipa mtendaji kata alimuita ofisini kwake akaambiwa alipe tena elfu 22,000
kama faini ambapo aliomba umda wa kuzitafuta.
Alisema alipoenda kutaka kuzilipa
aliomba apatiwe kwanz alisiti kutokana na malipo ya faini ya awali kufidia
hasara waliyoipata ndipo alipe faini nyingine ndipo utata ulipoanza na kwamba
aliamua kwenda Takukuru ili kupata haki yake huku akida serikali inasisitiza
risiti na yeye alitaka lisiti lakini viongozi hao hawakuwa tayari kumpatia.
Alisema baada ya kutoa taarifa
Takukuru walifika katika ofisi hiyo ya mtendaji kata ambapo walimchukua afisa
huyo hadi kwenye ofisi yao kwa ajili ya mahojiano na kilichoendelea huko
alisema hakukiju na kwamba usiku wake alishangaa askari mgambo kuanza kumsaka.
Hata hivyo maafisa hao wa Takukuru
Wilayani Rungwe hawakuwa tayari kulizungumzia suala hilo,wala kutaja majina yao
wakidai kuwa wao sio wasemaji na hata hivyo walisema wataharibu taratibu
zao za suchunguzi.
Kamanda wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) mkoani Mbeya Emmanuel Kiyabo hakupatikana
ofisini kwake kutokana na kuwa kwenye mapumziko mafupi ya mwishoni mwa wiki na
alipopigiwa simu iliita bila kupokelewa.
Akizungumza kwa njia ya
simu,Mwenyekiti wa hamashauri hiyo Ezekiel Mwakota,licha ya kukiri kuwepo na
hali hiyo,alisema chanzo ni mwanakijiji huyo, ambaye alikuwa akiwahamasisha
wafanyabiashara kutolipa ushuru baada ya halmashauri kubuni chanzo cha soko la
ndizi ambapo kila mgungu unalipiwa shilingi 100,na wanunuzi kutoka mikoani.
Alisema kwa sheria za halamashauri
ni kuwa kama mtu atazuia watu kulipa ushuru ni lazima atoe faini na kuwa
afisa mtendaji kumtoza faini mtu huyo alikuwa sahihi na kuwa baada ya hapo
kijana huyo alienda Takukuru ambao walikuja kuwachukua na kuwahoji.
Katibu Tawala wilayani Rungwe Moses
Mashaka,alisema hajapata taarifa kuhusu mtendaji huyo kuhojiwa na Taasisi
hiyo,na kwamba anachokijua ni kuhusu wenyeviti wa vitongoji na kijiji kutaka
kujiuzuru ambapo suala hilo linashughurikiwa na vyama vyao na wao wanasubiri
taarifa.
Hata hivyo,wenyeviti wa vitongoji na
kijiji hicho wamepanga kujiuzuru nyadhifa zao wakida kuwa afisa mtendaji huyo
anatumia vibaya ambapo wamesema hawapo tayari kufanya naye kazi wakidai amekuwa
na tuhuma lukuki.
Post a Comment