Header Ads


KUKITHIRI KWA MIMBA NA UTORO MASHULENI KWAWAPA CHANGAMOTO VIONGOZI



KYELA-MBEYA
ILI kudhibiti utolo na mimba za utotoni kwa wanafunzi,serikali
 wilayani Kyela mkoani Mbeya,imedhamilia kujenga Mabweni ili wanafuzi
 waweze kulala karibu na shule ambapo watakuwa katika uangalizi wa
 ahali juu lengo ni kuongeza ufauru.

 Hatua hiyo,imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi  ya wanafunzi
 kupata ujauzito wengine kutoudhuria kabisa masomo na kukosa kufanya
 mitihani ya kidato cha nne hali iliyopelekea serikali wilayani  humo
 imeweka mikakati ya kiukomesha hali hiyo.

 Miungoni mwa shule ambazo zimelipotiwa wanafunzi kupata ujauzito ni
 Itunge sekondari wanafunzi  wanne wa kidato cha nne hawakufanya
 mitihani baada ya kupatan ujauzito,shule zingine ni Katumba songwe
 sekondari na zinginezo,huku shule ya sekondari ya Masukila wanafunzi
 wanne walifukuzwa kwa kosa la kugoma kuimba wimbo wa Taifa.

 Kitendo cha wanafunzi hao wa kidato cha nne kugoma kuimba wimbo wa
 Taifa kiliwafukuzisha shule na kukosa kufanya mitihani huku wakidai
 dini yao hairuhusu kufanya hivyo kwa madai kuwa ni dhambi bila kujua
 kuwa kufanya hivyo ni kosa kwani wimbo wa Taifa unaimbwa na dini zote.

 Changamoto nyingine iliyopo kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule ni
 ukosefu wa usafiri hasa kwa shule mama ya Itope sekondari ambapo
 baadhi ya wanafunzi wanaishi umbali wa kilometa 15 ambao wanafika
 shuleni saa 2 na kurejea nyumbani saa 12 hadi saa 1 jioni kutokana na
 ukosefu wa usafiri.

 Kwa kutambua changamoto hizo,mkuu wa wilaya hiyo,Claudia Kitta,alisema
 serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo,imejipanga kujenga mabweni
 na kutoa elimu kwa wazazi kuona umuhinu wa watoto kuishi kwenye
 mabweni ili kuwalinda na mimba zisizotarajia.

 Kitta ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama,alisema
 watoto wanapotembea umbali mrefu kufuata elimu hasa wakati wa kurudi
 inakuwa ni majira mabaya wanakuwa katika hofu ya kubakwa na kupata
 mimba na kukatisha  ndoto zao za kimasomo.

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,Mussa Mgatta alisema
 ni kweli ukosefu wa mabweni ni chanzo wanafunzi kupata ujauzito na
 utoro,na kwamba wazazi hawana muamko wa kuwajali watoto wao kwani
 katika shule ya sekondari ya Itope upande wa pili lipo bweni lakini
 wanafunzi hawalali.

 Alisema kwa sasa wanajipanga  kwa kushirikiana na wadau  kujenga
 mabweni na kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuona umuhimu wa watoto
 kuishi katika mabweni hayo,na pia endapo mchakato huo utakamilika
 watakuwa na uhakika wa kupunguza mimba na utoro mashuleni.

No comments

Powered by Blogger.