Header Ads


JESHI LA POLI KANDA MAALUMU DAR ES SALAAM LIMEENDELEA KUFANYA MISAKO NA OPARESHENI KALI NCHINI




Naibu kamishna jeshi la polisi kanda maaalumu ya Dar es salaam Lucas Mkondya

DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm limeendelea kufanya misako na Oparesheni kali ambapo kuanzia tarehe 14/8/2017 mpaka tarehe 17/8/2017 limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 150 kwa makosa kubughudhi abiria katika maeneo mbalimbali ya ya jiji la Dsm katika stendi za mabasi kama ifuatavyo;
Stendi ya mabasi Ubungo walikamatwa watuhumiwa 39, posta watuhumiwa 12, Ferry watuhumiwa 7, Tegeta watuhumiwa 12, Tandika watuhumiwa 16, Mnazi mmoja watuhumiwa 6, Kituo cha daladala Stesheni watuhumiwa 5,Temeke Sterio 7,Gerezani 16, Manzese watuhumiwa 12,Bunju Bwatuhumiwa8, Kijiwe samli  watuhumiwa2na Buguruni watuhumiwa 3. Aidha watuhumiwa wote watapelekwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

WATUHUMIWA 167 WAKAMATWA JIJINI D’SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI YA KIHALIFU PAMOJA NA MADAWA YA KULEVYA KUANZIA TAREHE 11/8/2017 HADI 17/8/2017
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm limeendelea kufanya misako na Oparesheni kali ambapo kuanzia tarehe 11/8/2017 mpaka tarehe 17/8/2017 limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 167 kwa makosa mbalimbali  ya kiuhalifu. Makosa hayo ni: kupatikana na madawa za  kulevya, unyanga’nyi wa kutumia silaha/ nguvu, utapeli, wizi kutoka maungoni, kucheza kamari kuuza pombe haramu ya gongo, kupatikana na bhangi nk katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam .
Aidha katika oparesheni hii ambayo ni endelevu jumla ya Kete 96 za dawa za kulevya zimekamatwa, huku Puli zikiwa 87, Misokoto ya Bhangi 107, pamoja na pombe haramu ya gongo ipatayo lita 60.
Oparesheni hii kali ya kuwasaka wahalifu wa makosa hayo mbalimbali ikiwemo kosa la kupatikana na dawa za kulevya ni endelevu na hivyo raia wema wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi  ili kurahisisha kukamatwa kwa wahalifu hao na hatua kali za kisheria zifuate dhidi yao.
Watuhumiwa wote bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao na pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

POLISI KANDA MAALUM DSM KUPITIA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZIA TAREHE 11.08.2017 HADI TAREHE 17.08.2017 IMEFANIKIWA KUKUSANYA TSH 429,600,000 /=KWA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake  cha Usalama barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama  Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 11.08.2017 hadi tarehe 17.08.2017 ni kama ifuatavyo:-
        Idadi ya magari yaliyokamatwa                         - 13,712
        Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa                          - 749
        Daladala zilizokamatwa                               -5,701   
        Magari mengine (binafsi na malori)                        -8,335
     Bodaboda waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki                    -17
Jumla ya Makosa yaliyokamatwa                            - 14,461      
        Fedha za Tozo zilizopatikana                     –     429, 600,000 /=





                                                           L.J. MKONDYA- DCP
KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


No comments

Powered by Blogger.