JESHI LA POLISI DSM KUIMARISHA ULINZI MECHI YA NGAO YA HISANI KATI YA SIMBA NA YANGA ITAKAYOFANYIKA TAREHE 23/08/2017.
Naibu kamishna jeshi la polisi kanda maaalumu ya Dar es salaam Lucas Mkondya |
DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kwa kushirikiana
na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo
kati ya SIMBA na YANGA utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa unakuwa katika hali
ya usalama.
Aidha tunaomba wananchi wasiwe na wasiwasi wowote wa kiusalama
na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jambo lolote watakaloliona kuwa
linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa ndani
au nje ya uwanja.
Kutakuwa na CCTV Camera ili kuhakikisha sehemu zote za mageti ya kuingilia na kutokea na maeneo yote
yanaonekana na kuweka kumbukumbu za matukio yote.
Pia kutakuwa na askari kanzu watakaokuwa wanazunguka na kamera
pamoja na vinasa sauti (Tap recorder) kubaini matukio ya uhalifu, na yeyote
atakayebainika kuvunja sheria atashughulikiwa ipasavyo.
Pamoja na hayo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu katika
kushangilia mechi hiyo, na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:
•
Kuingia na chupa za maji,
•
Kuingia na silaha ya aina yoyote
•
Kupaki magari ndani ya uwanja
•
Kukaa sehemu ambazo tiketi zao
haziwaruhusu.
Mageti
yote yatafunguliwa saa tatu kamili asubuhi na muda huo mashabiki wataruhusiwa
kuingia uwanjani.
Post a Comment