Header Ads


LWANDAMINA- 'T'SHISHIMBI NI ZAIDI YA NIYONZIMA'


Kocha wa Yanga George Lwandamina amesema uwezo wa Niyonzima hauwezi kufikia kiwango alichokuwa nacho kiungo mpya Papii Tshishimbi
Kocha wa Yanga George Lwandamina amesema usajili wa kiungo Papii Tshishimbi umempa matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao.

Lwandamina ameiambia macheshazefrine.blogspot.com  kuwa anaitambua kazi ya kiungo huyo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo alikuwa anakipiga kwenye klabu ya Mbabane Swallows.
“Tshishimbi naweza kusema ni usajili bora kwangu, anakuja hapa kutibu tatizo letu la nafasi ya kiungo cha ukabaji; uwezo wake wa kupora mipira na kupiga pasi bado sijaona wa kumfananisha nae kwa Tanzania,”amesema Lwandamina.

Alisema kwamba shughuli ya Tshishimbi ndani ya uwanja inamuweka mbali na kiungo wa timu hiyo aliyetimkia Simba Haruna Niyonzima.
“Niyonzima alikuwa mahiri kwenye kuchezesha timu tu, lakini huyu anafanya kila kitu na zaidi anafunga mabao,”amesema Lwandamina.

Tshishimbi alimalizana na Yanga mapema wiki hii kwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili na ambapo anatarajiwa kukabidhiwa jezi nambari nane iliyokuwa ikivaliwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Amesema uwezo wa Tshishimbi wa kukaba na kusukuma mashambulizi unamfanya apate cha kuvijunia na kusisitiza kuwa atakuwa na ushirikiano mzuri na kiungo mwingine wa timu hiyo Thabani Kamusoko.

No comments

Powered by Blogger.