Header Ads


Asilimia 45 ya wakenya wasema watapigia kura wagombea huru

Asilimia 45 ya wakenya wasema watapigia kura wagombea huru
mlolongo wa wapiga kura
Aslimia 45 ya wakenya wanasema watawapigia kura wagombea huru kwenye uchaguzi wa Agosti nane huku aslimia 46 wakisema watapigia kura wagombea walio katika vyama. Hii ni kulingana na utafiti ulioendeshwa na kituo cha African Progress unaonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wana umaarufu wa aslimia 53 dhidi ya aslimia 42 ya mgombea wa NASA Raila Odinga na mgombea mwenza wake kalonzo musyoka. Utafiti huo ulioendeshwa kati ya tarehe 24 hadi 27 unaonyesha kuwa aslimia 52 ya wakenya wana imani katika utendakazi wa tume ya IEBC kuandaa uchaguzi huru na wa amani huku aslimia 45 wakitilia shaka.

No comments

Powered by Blogger.