WANANCHI WA KIJIJI CHA SAMAZI WILAYANI KALAMBO MKOANI RUKWA WALALAMIKIA ZAHANATI YAO
RUKWA-KALAMBO
Na.baraka lusajo
WANANCHI wa kijiji cha
Samazi katika mwambao
wa ziwa Tanganyika wilaya
ya Kalambo Mkoani Ruwa, wamelalamikia kitendo cha zahanati ya
kijiji hicho kuwa
na ukosefu wa
madawa kwa zaidi ya
mwaka mmoja na
wakati walilipia mfuko
wa bima ya afya
CHF tangia mwaka
jana kiasi cha
shilingi milioni moja (1,000,000/=).
Kwa lengo la kuepukana
na swala la
kununua madawa kwenye maduka
ya dawa.
Hatua hiyo
inakuja baada ya
wananachi hao kujitoa kwa
moyo katika kuchangia
mfuko wa bima
ya afya CHF na
kuchangia kiasi
cha shilingi elfu
kumi kwa kila
mmoja na kushanga
baada ya wahudumu
wa afya kwenye Zahanati hiyo kuwatuma
kununua madawa kwenye
maduka na wakati walikwisha
kuchangia fedha za
CHF tangia mwaka
jana na kuomba serikali
kupitia idara ya afya
kuingilia kati swala
hilo.
Mwenyekiti wa
kamati ya afya
kijijini hapo, amosi
Mazinga , amesema walitoa oda
ya dawa tangia
mwaka jana kupitia
idara ya afya
lakini cha kushanagaza
mpaka leo hawajazipata.
Kaimu mganaga mkuu
wa wilaya humo
Andondile mwakilima , ambae
licha ya kukili
wazi kuwepo adha
ahiyo amesema atalifikisha
swala hilo kwa
mganga mkuu wa
wilaya ili kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia
wananchi hao kupata dawa
mapema.
Post a Comment