Header Ads


ANAYE DAIWA KUWA DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MUHIMBIRI JIJINI DAR ES SALAAM



DAR ES SALAAM
Walinzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (MNH) wamemnasa mtu
mmoja ambaye inadaiwa amekuwa akijifanya daktari na kuwarubuni wagonjwa.

Walinzi wa hospitalini hapo walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu lakini
leo Jumatatu ndiyo wamemnasa akiwa katika harakati za kufanya
kinachodhaniwa kuwa ni utapeli.

Abdala Juma (30) alikamatwa kwenye viunga vya hospitali hiyo akizungumza
na ndugu wa wagonjwa waliofika kuchangia damu huku akiwa na kifaa cha
kupimia mapigo ya moyo kinachoning'inizwa shingoni na madaktari.

Akizungumza na Mwananchi, Juma alisema alifika hospitalini hapo
kumsalimia rafiki yake lakini alishangaa akikamatwa na kuwekwa chini ya
ulinzi.                      

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiliel Aligaesha amesema
kukamatwa kwa mtu huyo ni mwendelezo wa mikakati waliyoiweka kupambana
na vishoka.

No comments

Powered by Blogger.