ZAHANATI ZA WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA ZA KUMBWA NA UHABA WA MADAWA
Zahanati |
KALAMBO-RUKWA
IMEELEZWA
kuwa kukosekana kwa dawa
kwenye vituo vya afya na zahanati katika
wilaya ya kalambo mkoani Rukwa
ni kutokana na wakuu wa idara
ya afya kushindwa kutoa taarifa mapema
kwenye uongozi husika pamoja na
kushindwa kujua bajeti ya dawa kwenye
vituo vyao na kupelekea kujitokeza
kwa malumbano baina yao na wananchi.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akiongea na
wahudumu wa afya katika wilaya
ya kalambo mkoani hapa, ambapo ameshangazwa
na kitendo cha kusekana kwa
dawa kwenye vituo vya afya na
zahanati wilayani humo kutokana na
serikali kuongeza bajeti ya fedha za
dawa katika wilaya hiyo kutoka
milion 121 hadi kufikia
shilingi milioni 333 .
Amesema kituo
cha afya cha Matai pekee ambacho
kinatoa huduma kama hospitali ya
wilaya kimeongezewa bajeti kutoka
shilingi laki mbili na sabini na
sita hadi kufikia kiasi
cha shilingi milioni mbili na laki
sita na kuwa fedha hizo
zimetolewa kwa ajili ya dawa pekee na
kuwagiza madiwani kusimamia fedha hizo ili
zitumike kama ilivyopangwa.
Kwa upande wa
wahudumu wa afya wilayani humo wameiomba
serikali kuwaongezea mishahara hususani kwa
watumishi ambao wamekuwa wakiongezea
elimu yao sambamba na kuwapandisha madaraja
kwa wakati ili kuongeza jitihada ya
ufanisi wa kazi.
Post a Comment