TETESI ZA USAJILI LEO 27.7.2017
Macheshazefrine.blogspot.com inakuletea muhtasari wa tetesi na habari za uhamisho kutoka Ligi Kuu Uingereza, La Liga, Serie A, Bundesliga na kwingineko
REAL YAKUBALI KULIPA €180M KUMSAJILI MBAPPE
Real Madrid imefikia makubaliano na Monaco kuhusu ada ya euro milioni 180 kumsajili kinda matata Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Marca .
Uhamisho huo wa rekodi utakapofanyika, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa atasaini mkataba wa miaka sita kujiunga na Mabingwa hao wa La Liga.
ARSENAL WANAKARIBIA KUMSAJILI LEMAR KWA £45M
Hatimaye Arsenal wanakaribia kukamilisha dili la usajili wa winga wa Monaco Thomas Lemar kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 45 kwa mujibu wa The Sun.
Monaco walishakataa ofa kumuuza Lemar na walitaka kumzuia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kujiunga na Washika Mtutu wa London, lakini Arsenal inaaminika wamewashawishi mabingwa hao wa Ligue 1 kumuuza.
STOKE YAZUNGUMZA NA OXLADE-CHAMBERLAIN
Stoke City inafanya mazungumzo na wakala wa Alex Oxlade-Chamberlain kuhusu ada ya £25 millioni kwa ajili ya kiungo huyo wa Arsenal kwa mujibu wa The Sun .
BRIGHTON YAMSAJILI KINDA WA CHELSEA
Brighton & Hove Albion wameshinda mbio za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Izzy Brown kwa uhamisho wa mkopo, kwa mujibu wa The Argus .
BARCA YAKARIBIA KUMSAJILI COUTINHO KWA €100M
Viongozi wa Barcelona wapo mjini London katika harakati za kukamilisha uhamisho wa nyota wa Liverpool Philippe Coutinho, Sport kimeripoti.
Mazungumzo yamekuwa mepesi lakini klabu hiyo ya Hispania italazimika kulipa kitita cha euro milioni 100 kumsajili nyota huyo wa Liverpool.
ARSENAL & LIVERPOOL ZINAMKODOLEA BENZEMA
Arsenal na Liverpool zinaweza kufanya harakati za kumsajili Karim Benzema ikiwa Real Madrid watakuwa tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa Kifaransa Don Balon limeripoti.
BARCA IMEKATAA OFA YA ROMA KWA AJILI YA MUNIR
Barcelona wamekataa ofa ya euro milioni 25 kutoka Roma kwa ajili ya Munir El Haddadi, kwa mujibu wa Sport .
Miamba hao wa Serie A wanaangalia mchezaji wa kusajili ikiwa mipango yao kumsajili Riyad Mahrez itagonga mwamba na wamepanga kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini miamba wa Catalan wanahitaji fedha ndefu.
PEREZ HUENDA AKAPEWA NAFASI YA KUTOROKA ARSENAL
Bayer Leverkusen na Marseille zinatamani kuipata huduma ya mchezaji wa Arsenal alieychoka kusugua benchi Lucas Perez, kwa mujibu wa The Sun .
Perez anatamani kuondoka Arsenal ili apate fursa ya kucheza kikosi cha kwanza na klabu yake ya zamani Deportivo La Coruna pia inatamani huduma yake.
VITA YA £8M KWA AJILI YA MARKOVIC
Hull City na Watford zinapigana vikumbo kuiwania saini ya winga wa Liverpool Lazar Markovic kwa dili ya paundi milioni 8, kwa mujibu wa The Sun .
Liverpool wapo tayari kupokea paundi milioni 13 kumuuza Mserbia huyo ambaye ametumika nusu msimu kwa mkopo Hull msimu uliopita.
CAN AKUBALI OFA YA JUVE
Emre Can amefikia makubaliano ya masharti binafsi baina yake na Juventus ili kuondoka Liverpool kujiunga na mabingwa hao wa Serie A, kwa mujibu wa TMW .
DEMBELE AIPA NAFASI KUBWA REAL KUMSAJILI
Winga wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele anataka kutua Real Madrid uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa Don Balon .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekata tamaa kutua Barcelona na badala yake anafikiria kujiunga na mabingwa wa La Liga.
Post a Comment