KOCHA ZUBEIR KATWILA AMEONYESHA KULIDHISHWA NA MWENENDO WA TIMU YAKE
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Zubeir
Katwila ameonyesha kuridhishwa na mwenendo wa maandalizi ya kikosi chake
ambacho kwa sasa kimeweka kambi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiwinda na
mshike mshike wa ligi kuu ambao utaanza rasmi August 26.
Katwila amesema tangu walipoanza
maandalizi ya ufukweni na kufikia hatua ya kuchezo michezo ya kirafiki, ameanza
kuona lengo alilolikusudia kwa ajili ya msimu ujao linaanza kutimia kwa
asilimia kadhaa.
Kocha huyo ambaye alikabidhiwa majukuu
ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi mara baada ya kuondoka kwa Salum Shaban
Mayanga aliyeteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) pia
amezungumzia usajili wa kiungo Hassan Dilunga aliyetokea kwa maafande wa JKT
Ruvu ambao msimu ujao watashiriki ligi daraja la kwanza.
Wakati huo huo Katwila amesifia uwezo
wa wacvhezaji chipukizi ambao amewapendekeza kuongezwa katika kikosi cha kwanza
kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na tayari ameanza kuwatumia kwenye michezo ya
kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.
Mlinda mlango Shaaban Kado amefichua
siri ya kilichomrejeshwa Mtibwa Sugar katika kipindi hiki cha usajili, akitokea
Mwadui FC ambao amewatumikia kwa misimu miwiwli iliyopita.\
KAdo ambaye alikua mtibwa Sugar kabla
ya kutimkia kwa mabingwa wa Tanznaia bara young Africans na kisha mkoani
Shinyanga yalipo makao makuu ya Mwadui FC, amesema jambo kubwa lililomrejesha
kati kati ta mashamba ya miwa ni ukaribu uliopo kati yake na viongozi wa Mtibwa
Sugar pamoja na mazingira ya ufanyaji kazi klabuni hapo.
Post a Comment