MAAMUZI YA CAF YAIUMIZA ZANZIBAR
Maamuzi ya shirikisho la soka barani
Afrika CAF ya kuiondoa Zanzibar kwenye uanachama, yameendelea kuwa gumzo
kisiwani Unguja huku kila mdau aliyezungumza na kipindi hiki akikiri
kuhuzunishwa na kilichoamuliwa na shirtikisho hilo.
Mmoja wa wadau wa soka tuliozungumza
nao ni aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum
Bausi ambapo amesema suala la CAF kuwaengua kwenye uanachama limemuhuzunisha
kutokana na fursa waliokua wameipata ya kucheza michuano ya kimataifa kupitia
klabu za soka visiwani humo kuondoshwa.
hivyo Bausi ametoa sababu ambazo
anaamini huenda zikawa zimechangia Zanzibar kupokonywa uanachama wake ambao
ulidumu kwa miezi minne tangu walipoupata mapema mwaka huu.
Sababu nyingine iliyotajwa na Bausi
ambaye pia alijaribu kuwania nafasi ya urais wa chama cha soka visiwani
Zanzibar miaka miwili iliyopita, ni maamuzi ya viongozi wa ZFA ambayo amekiri
hayakuwa na busara dhidi ya wadau wa soka visiwani humo.
Baada ya kuzungumza mambo hayia mabayo
anaamini yalikua kichocheo cha Zanzibar kupokonywa uanachama wake, Bausi akatoa
ushauri kwa viongozi wa chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA ili kulinusuru
soka la visiwa hivyo vya Afrika mashariki.
Post a Comment