MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKABIDHI KOMPUTA 50 KWA MANSPAA TANO ZA JIJI LA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Computer za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilling Million 170 kwa Manispaa tano za Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Watu wa Jiji na Mkoa kwaajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.
Ikumbukwe, Tarehe 18 mei mwaka huu mkuu wa huo alipokuwa akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na ujenzi kutoka katika manispaa ya ubungo,kigamboni,ilala,kinondoni na temekena halmashauri ya jiji la Dar es salaam,ambapo Alisema Ardhi Na Ujenzi ni moja Kati ya Idara zenye matatizo mengi katika Mkoa wa Dar es salaam hivyo alitoa msisitizo kwa vibali vya Ujenzi kutolewa haraka ndani ya mwaka mmoja kwani kuchelewesha kunapelekea wananchi wengi kujenga bila utaratibu.
Watumishi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam wakichangamkia kompyuta walizopatiwa kwaajiri ya kuwarahishia kazi katika suala la utoaji vibali vya ujenzi jijini Dar es salaam leo jijini Dar es salaam. |
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alitoa maelekezo 17 ya kuzingatia kwa watendaji wa Sekta hiyo ya Ardhi Na Ujenzi ambayo ni pamoja Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu, Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017 huku Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kukitarajiwa kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.
Aidha siku ya leo ya tarehe 27 july 2017 amefanya mgawanyo kwa kila Manispaa kupatiwa Computer nane huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa Computer tano na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa Computer tano ikiwa ni ufadhili wa kampun ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono Mheshimiwa Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.
Baadhi ya kompyuta zilizo tolewa na TAMOBA ka wilaya za mkoa wa Dar es salaam leo hii. |
Makonda amesema Computer hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi ambapo mwananchi atakuwa na uwezo wa kutuma maombi ya kibali cha ujenzi kwa kutumia simu ya mkononi ke au Computer hata akiwa nyumbani na akapewa majibu yake kwa haraka.
“Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso,malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya kero ya Ardhi, na namna mbili ya kupunguza ni kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dr.John Magufuli, namna ya pili ni kusimamia uwajibikaji kwamba kila mmja anatekeleza majukumu yake ili Mwananchi wa Mkoa wa Dar es salaam asipate adha na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye Sekta ya Ardhi, umuhimu wa kutoa vibali vya ujenzi ni muhimu katika mji huu unaokuwa kwa kasi barani Afrika” Alisema Makonda.
Computer hizo zitawekewa Mfumo maalumu utakaokuwa ukikusanya Maoni na mapendekezo ya wananchi ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kutuma maoni yao na kero mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta ya Ardhi.
Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda akishughulika katika kushusha kompyuta zitakazo saidiawilaya za Dar es salaam katika kutoa vibali kwa haraka kwa wananchi wa Dar es salaam leo. |
“Tumeishi sana kwenye mfumo wa makaratasi na mafaili, na wakati mwingine kumekuwa na changamoto ya kupotea kwa mafaili na mwananchi kupata adha ya kutoelewa nini afanye maana ataanza upya kutuma maombi, lakini sio hivyo inafanya kazi kuwa ngumu, pia ni chanzo cha rushwa pale mwananchi anapokuwa akisumbuliwa na mtumishi, naamini Compuer hizi zinaenda kukata mzizi wa fitina, Wananchi kulundikana ofisini ni kero kubwa, wananchi kusumbuka kupata huduma ni kero kubwa”, Alisema Makonda.
Post a Comment