WAKUU WA IDARA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA WILAYANI MOMBA MKOANI SONGWE WAMEONYWA KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUKAIMISHA VYEO VYAO
Kuria :aliye shika mic mkuu wa wilaya ya momba juma said |
Momba-Songwe
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya momba Juma Saidi
Irando katika kikao maalumu cha hoja za
CAG kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa tunduma ambapo
amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi wanakaimisha nafasi zao wakati wa ukaguzi
wa hesabu za serikali na kuonya kuacha tabia hiyo mara moja na atakaye kaidi agizo
hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha Irando ameongeza kuwa kuna hoja ambazo
zinatakiwa mkuu wa idara azijibie na si kukaimisha vyeo halafu zinaanza kuibuka
hoja kwa mkaguzi kitu ambacho hakitakiwi hivyo watumishi wote wafuate taratibu na sheria.
Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa songwe Eliya
Ntandu amesema kuwa watumishi wote wa
serikali wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo amewataka waache kufanya
kazi kwa mazoea lakini pia waheshimu sheria zilizowekwa ili kupeleka maendeleo
mbele ambapo amesema kuwa asingependa hoja zilizotolewa zijirudie tena.
Post a Comment