KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUKUTANA LEO
Kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF leo inatarajia kukutana kwa
ajili ya kupitia rufaa za wadau wa soka walioenguliwa kwenye mchakato wa
uchaguzi wa shirikisho hilo ambao utahitimishwa August 12 kwa wajumbe wa
mkutano mkuu kupiga kura.
Afisa
habari wa TFF Alfred Lucas amesema mpaka sasa wadau watatu ndio waliowasilisha
rufaa zao ambazo zinapinga maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya uchaguzi
inayoongozwa na wakili Msomi Levocutus Kuuli.
Hata hivyo Shafii
Dauda amefikia hatua ya kutangaza kujiengua kuwani nafasi hgiyo kufuatia sakata
la kudaiwa kujihusisha na utoaji wa rushwa mwanzoni mwa juma hili na kupelekea
kuhojiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa tawi la mkoa wa Mwanza
alipokua amekwenda kwa shughuli binafsi.
Wakati huhuo Shirikisho la soka nchini TFF limeendelea kuwasisitiza mabingwa wa
soka Tanzania bara Young Africans kuhusu uhalali wa usajili wa aliyekua mlinda
mlango wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys)
wakati wa faianli za Afrika zilizofanyika nchini Gabon mwezi Mei Ramadhan
Kabwili.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema wanaendelea kutoa
msisitiz huo kutokana na kutokua na uhakika wa usajili wa mlinda mlango huyo
umengukia kwenye kikosi cha wakubwa ama vijana cha klabu hiyo, hivyo wanapaswa
kuwa makini kutokana na umri wa mchezaji huyo kuwa chini ya miaka 18.
Hata
hivyo Alfred amesema wanaendelea kusubiri mkataba uliosainiwa na Ramadhan
Kabwili kwa makubaliano na viongozi wa Young Africans ili kujiridhisha zaidi.
Post a Comment