MAUWAJI MKOANI RUKWA YAMEZIDI KUONGEZEKA KWA KASI.
SUMBAWANGA-RUKWA
MWANAMKE
aliyefahamika kwa jina la Anna Kashamakula(40) ameuawa kwa kuchomwa kisu na
mumewe wake baada ya kumhoji kuhusiana na mwanaume huyo kuchukua fedha za
kulipia kodi ya nyumba wanayoishi kiasi cha shilingi 30,000 na kudaiwa kwenda
kula raha na hawara yake.
Tukio
likitokea jana majira ya saa 6 za usiku katika kitongoji cha Mafulala mjini
Sumbawanga baada ya kuibuka mzozo baina ya wanandoa hao ambapo mke alimtuhumu
mume wake kuwa amechukua fedha hizo ambazo yeye amezipata baada ya
kufanya biashara ndogo ndogo na kisha kwenda kuzitumbua na hawara yake.
Akizungumzia
tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Mafulala,Christopha Kalingi alisema kuwa
kabla ya mauaji hayo ulizuka mzozo baina ya wanandoa hao ambapo marehemu
alikuwa akimtuhumu mumewake huyo kuwa amechukua fedha hizo na kwenda kula raha
na hawara yake.
Baada
ya mzozo wa muda mrefu ndipo mtuhumiwa huyo alipokasirika na kwenda kwenye
chumba cha watoto wao na kuwafungia mlango kwa nje na kisha kuamua kumpiga mke
wake na kumchoma kisu tumboni na kumsababishia jeraha kubwa lililosababisha
kuvuja kwa damu nyingi.
Baada
ya kutenda tendo hilo mtuhumiwa alikimbia na kwenda kujificha porini, ambapo
baada ya tukio hilo watoto wa wanandoa hao walipiga kelele za kuomba msaada
ndipo majirani walipofika ili kumkimbiza mwanamke huyo hospitali kwaajili ya
matibabu.
Mwenyekiti
Kalingi alisema kuwa kutokana na kuwa tukio hilo lilitendeka nyakati za usiku
na ilikuwa tabu kupata usafiri wa kumuwaisha hospitali majeruhi kitendo
kilichosababisha avuje damu nyingi kwenye jeraha lake na kufariki dunia wakati
wakiwa njiani wakimuwahisha hospitali kwaajili ya matibabu.
Asubuhi
polisi walipo anza kufanya msako ndipo walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa
amejificha porini na anashikiliwa na polisi ambapo anatarajiwa kufikishwa
mahakamani baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
Kamanda
wa polisi mkoani Rukwa George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuwaonya wakazi wa mkoa huo kuacha tabia ya kunywa pombe kupita kiasi pamoja na
uvutaji wa bangi kwani vitu hivyo vimekuwa vikiwasababisha wakazi wa mkoa huo
kutenda matukio ya uhalifu mara kwa mara na kuwasihi kushirikisha ndugu na
jamaa katika kutatua matatizo ya kifamilia kuliko kujichukulia sheria
mkononi.
Post a Comment