MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA RENATUS NJOHORE ATOA WASIA KWA VIJANA
Mtanzania aliyefanikiwa kucheza soka nchini Uswiz Renatus Njohole
ametoa ushauri kwa wachezaji wenye ndoto za kucheza soka nje ya nchi kwa
kuwaambia wasikatishwe tama na mazingira watakayokwenda kukytana nayo.
Njohole
ambaye aliitumikia timu ya taifa mara kadhaa wakati w autawala wa kocha kutoka
nchini Brazil Marcio Maximo amesema soka la nje ya nchi limekua na changamoto
kubwa sana kwa wachezjai kutoka barani Afrika, hususana katika nchi ambazo
hazifahamiki kama Tanzania, hivyo kwa mchezaji yoyote kutoka hapa nchini kama
atatimiza malengo hana budi kupambana na kukubaliana na changamoto ztakazo
kutana nazo.
Hata
hivyo Njohole ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Simba wakati akiwa hapa nchini
amekiri kufurahishwa na mwenendo mzuri wa soka la Tanzania kwa kusema limeanza
kuonyesha mabadiliko taratibu taratibu.
Hata
hivyo Njohole amesema soka la barani Ulaya hususan katika nchi ya Uswiz ambapo
ndipo makazi yake yalipo kwa sasa, kwa kusema limekua na nafasi kwa yoyote
anaetaka kwenda huko kucheza, lakini cha kuzingatia zaidi ni suala la nidhamu
ambayo imekua ikitazamwa kama silaha kubwa ya mafanikio duniani kote.
Post a Comment