Header Ads


MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALAWA AMEWATAKA MAOFISA KILIMO KUHAKIKISHA TATIZO LA UWEPO WA KIWAVI JESHI KATIKA BAADHI YA WILAYA MKOANI HAPA LINAISHA







Mbozi
Mkuu wa mkoa wa songwe chiku galawa amewataka maofisa kilimo na maofisa ugani mkoani hapa kuhakikisha wanaharakisha kumaliza tatizo la uwepo wa kiwavi jeshi ambaye ameanza kuharibu mazao mbali mbali ya wakulima.
Galawa  ameyasema hayo katika kikao cha ushauri kilichowakutanisha wajumbe mbali mbali  kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya mbozi ambapo amewataka viongozi hao kuharikisha kudhibiti tatizo hilo kabla halijaathiri maeneo mengi kwani asilimia kubwa ya wakulima wa songwe wanategemea kilimo.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti wa halimasahauri ya wilaya ya mbozi Erick ambakisye amesema mdudu huyo ni hatari ambapo ametaka taarifa ziwe zinatolewa mapema pindi mkulima anapomuona mdudu huyo ili kumdhibiti mapema na kuwataka wakulimakuongeza uzalishaji ili suala la njaa katika wilaya ya mbozi ibaki historia.
Hatua hiyo imekuja baada ya mshauri wa kilimo mkoani hapa vanska kulanga  kuzungumzia uwepo wa kiwavi jeshi katika wilaya za momba, mbozi na ileje ambapo amesema mdudu huyo tayari ameanza kushambulia mazao katika baadhi ya mashamba ya wakulima katika wilaya hizo.
Aidha Kulanga ameshauri wakulima kujenga utamaduni wa kutembelea mashamba yao mara kwa mara ili mabadiliko yoyote katika mazao au mdudu huyo wanatoa taarifa kwa wataalamu ili kudhibiti mapema.

No comments

Powered by Blogger.