SERIKALI MKOANI RUKWA IMESITISHA SHUGHULI ZOTE ZA UVUVI KATIKA ZIWA RUKWA KWA MUDA USIOJULIKANA
Rukwa
SERIKALI
mkoani Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwamuda usio julikana kutokana
na shughuli za uvuvi kuchungia kasi ya ugonjwa wa kipindupindu katika ziwa
hilo.
Mkuu wamkoa huo Joachim Wangabo
alitoa agizo hilo wakati akizingumza na wavuvi kwa lengo lakuwaeleza sababu za
kulifunga ziwa hilo na kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea.
Amesema kuwa baada ya kukaa na
wataalamu wa afya wamekubaliana kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa
chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa huo.
Amesema kuwa athari inayopatikana
katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri wala samaki wanaotokana ziwa hilo hasa
waliopo Sumbawanga mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kitoweo na kuwataka
waliopiga kambi katika ziwa hilo kwaajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani
hawata ruhusiwa kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki.
Aidha ameagiza kufunguliwa maeneo
maalumu kwaajili ya kuwatibia wagonjwa watakao patikana kwani wasipofanya
hivyo mlipuko wa ugonjwa huo utaendelea kuongezeka na watu wengi zaidi
wataendelea kupoteza maisha kwa ugonjwa huo.
Mkuu huyo wa mkoa alifanya
ziara katika kambi ya wavuvi ya mererani iliyopo katika kijiji cha
Ilanga, Kata ya Muze Wilaya ya Sumbawanga katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo
mpaka sasa Jumla ya wagonjwa 9 waliripotiwa kuugua kipindupindu.
Awali akitoa taarifa ya ugonjwa huo
Afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Plasidus Malapwa alisema kuwa
ugonjwa huo ulibainika tangu novemba 23 kutokana na mgonjwa aliyetoka kambi ya
Lichili, Kijiji cha Lichili, wilayani Momba, Mkoani Songwe na kufia katika
kambi ya kamchanga, Kata ya Muze, wilayani Sumbawanga na kuanzia hapo wagonjwa
walianza kuongezeka hali iliyosababisha kuanzishwa kwa kambi nne kuzunguka ziwa
Rukwa.
Post a Comment