MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALAWA AMEAGIZA MAOFISA KILIMO MKOANI HAPA KUHAKIKISHA WANALIMALIZA TATIZO LA UWEPO WA KIWAVI JESHI KATIKA MASHAMBA YA WAKULIMA
SONGWE
Mkuu
wa mkoa wa songwe chiku galawa amewataka maofisa kilimo na maofisa ugani mkoani
hapa kuhakikisha wanaharakisha kumaliza tatizo la uwepo wa kiwavi jeshi ambaye
ameanza kuharibu mazao mbali mbali ya wakulima.
Galawa
ameyasema hayo katika kikao cha ushauri kilichowakutanisha wajumbe mbali
mbali kilichofanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya ya mbozi ambapo amewataka viongozi hao kuharikisha
kudhibiti tatizo hilo kabla halijaathiri maeneo mengi kwani asilimia kubwa ya
wakulima wa songwe wanategemea kilimo.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti
wa halimasahauri ya wilaya ya mbozi Erick ambakisye amesema mdudu huyo ni
hatari ambapo ametaka taarifa ziwe zinatolewa mapema pindi mkulima anapomuona
mdudu huyo ili kumdhibiti mapema na kuwataka wakulimakuongeza uzalishaji ili
suala la njaa katika wilaya ya mbozi ibaki historia.
Hatua hiyo imekuja baada ya mshauri wa kilimo mkoani
hapa vanska kulanga kuzungumzia uwepo wa
kiwavi jeshi katika wilaya za momba, mbozi na ileje ambapo amesema mdudu huyo
tayari ameanza kushambulia mazao katika baadhi ya mashamba ya wakulima katika
wilaya hizo.
Aidha Kulanga ameshauri wakulima kujenga utamaduni
wa kutembelea mashamba yao mara kwa mara ili mabadiliko yoyote katika mazao au
mdudu huyo wanatoa taarifa kwa wataalamu ili kudhibiti mapema.
Post a Comment