ZAIDI YA NYUMBA70 ZABOMOLEWA NA KUHARIBIWA VIBAYA KATIKA KATA YA IVUNA WILAYA YA MOMBA
MOMBA
Zaidi
ya nyumba 70 zimebomolewa na kuharibiwa vibaya katika vijiji vitatu vilivyopo
kata ya ivuna wilaya ya momba mkoani hapa baada ya mvua kubwa kunyesha
iliyokuwa imeambatana na upepo mkali.
Vijiji vilivyokumbwa na janga hilo ni kijiji cha
itumbula kalungu iwatwe na samang’ombe ambapo wakaazi wa maeneo hayo wamesema
wanahofia kuwepo kwa njaa kali kutokana na mvua hiyo licha ya kubomoa nyumba
zao na nyingine kuezuliwa zimeharibu pia vyakula vya akiba kutokona na kuingia
maji.
Aidha wameiomba serikali kuwachukulia hatua wale
wote ambao wamekua wakivamia maeneo ya misitu kulima kwakua hatua hiyo
inasababisha kuwepo kwa tatizo hilo kutokana kwamba uwepo wa miti unasaidia
kuzuia upepo mkali ambao unaweza ukaleta maafa ikiwa ni pamoja na kuezua
nyumba.
Kufuatia hatua hiyo mkurugenzi wa halimashauri ya
wilaya ya momba adriani jungu alitembelea vijiji hivyo na kutoa pole kwa waathirika
na kusema kama serikali watasaidia kuwapatia chakula na kutoa wito kwa majirani wa
waathirika kuweza kuwasitili kwa muda wakati serikali inaendelea na taratibu
nyingine na kuwasaidia.
Aidha amesema wataimarisha huduma za afya kwani
yanapotokea maafa kama hayo huwa kunakuwepo na magonjwa na milipuko na kutoa
wito kwa wananchi hususani wakulima na wafugaji kuacha kuvamia maeneo ya misitu
kwani ni moja kati ya sababu zinazopelekea maafa kama hayo na kuahidi kuwaondoa
wote, lakini pia ametoa wito kwa wananchi kupanda miti badala ya kukata.
Post a Comment