Header Ads


MADIWANI KATIKA HALIMASHAURI YA WILAYA YA MBOMBA MKOANI HAPA JANA WAMETUNGUA KAULI YAO RASIMI YA KUTOKUSHIRIKIANA NA MKUU WA WILAYA HIYO






 MOMBA 
MADIWANI katika halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe,jana wametengua na kuomba radhi mbele ya mkutano wa hadhara wa wananchi  juu ya kauli waliyoitoa ya kuvunja mahusiano na mkuu wa wilaya hiyo Juma Irando.
Hatua hiyo ya kuomba radhi na kutengua kauli imekuja baada ya siku tano zilizopita kufanya hivyo ambapo serikali haikuridhika na namna walivyotengua kauli,kwenye uwanja ambao haukutumika kutolea kauli walitakiwa kuitisha mkutano kwenye uwanja uliotumika awali wakati wa kutoa tamko,eneo la uwanja wa shule ya msingi Tunduma..
Akizungumza jana kwenye mkutano huo,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ally Mwafongo,alisema Tarehe 18/9/2017 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri,madiwani 13 na viti maalum jumla 19 walitengua mahusiano na mkuu wa wilaya kwa madai ya kukiuka taratibu za kiutandaji ambapo diwani 1 pekee aliyotokana na ccm hakuhusika..
Alisema kitendo cha mkuu wa wilaya kutumia nguvu kuwafukuza wafanyabiashara wadogo (Machinga) kwenye maeneo yao pasipo kuwatafutia maeneo mbadara na rafiki pasipo wao kushirikishwa kiliwaumiza ambapo waliazimia kuondoa ushirikiano naye wakidhani Rais Magufuli anamuondoa na atampeleka Mkuu wa wilaya mungine.
Alisema baada ya kauli hiyo walilazimika pia kuwaeleza wenyeviti wa serikali zote 71 za mitaa kutoashirikiana na mkuu huyo,ambapo alisema tamko hilo lilizua taharuki ambapo serikali imatafsili vibaya kuwa wao wanaikataa serikali kuu.
Aliongeza kuwa wao walimkataa mkuu huyo,Juma Irando kwa matendo yake hawakuikataa serikali kuu na ndiyo maana wamekuwa washirikiana na mkuu wa mkoa Chiku Galawa kwenye ziara zake na kuwa hata mkuu wa mkoa Kassim Majaliwa alipofika walimpa ushirikiano wa kutosha ambapo Tunduma ilivunja rekodi katika mapokezi yake.
Alisema baada ya kuona shughuri za maendeleo zinasuasua huku wakipokea ushauri wa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wakubwa serikalini pamoja na vyama vyote vya siasa kuwa watengue kauli hiyo ili shughuri za kijamii ziendelee walikubali kufanya hivyo na kuitengua kauli hiyo na kumuomba radhi mkuu huyo.
Herode Jivava diwani wa kata ya Tunduma,ambaye poia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,alisema kauli hiyo imetafsiliwa vibaya ikaonekana kuwa wao hawaitambui serikali,hivyo wanaomba radhi na kutengua kauli hiyo ili kurudisha mahusiano na kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa masrahi ya wananchi waliowachagua..
Bonifas Mwakabanje,mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Tunduma,alisema wametafakari mambo mengi na kutoa ushauri kwa madiwani hao kutengua kauli ili kurudisha mahusiano na mkuu wa wilaya kwa kuwa muungano wa madiwani na watendaji ni muhimu kwa mustakabari wa kiutendaji.
Akizungumza kwaniaba ya wananchi wa Tunduma,Julias Mwavilenga,alisema mgogoro huo,umeathiri shughuri nyingi za maendeleo,zikiwemo ujenzi wa shule,zahanati na zinginezo na kwamba kurudishwa kwa mahusiano mutairejesha Tunduma katika kasi yake ya maendeleo iliyokuwa inakuja kwa kasi.
Awali akizungumza katika mikutano ya hadhara,baada ya wananchi kuomba mahusiano yarejee,mkuu wa wilaya hiyo Juma Irando,alisema madiwani ndiyo waliotengua mahusiano,ambapo nayeye amewaagiza watendaji kutoshirikiana nao na kwamba wao wanatakiwa kutengua kauli na wakifanya hivyo hata kuwa na kinyongo kufanya nao kazi.

No comments

Powered by Blogger.