NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA TAMISEMI JOSEPHAT KANDEGE AMEWAAGIZA VIONGOZI MKOANI RUKWA KUWAONDOLEWA WANANCHI DHANA KWA SERIKALI ITAWALETEA MAENDELEO
RUKWA
Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala
za mikoa,( Tamisemi )Josephat Kandege amewaambia watumishi wa umma mkoani Rukwa
wawaondolee dhana wananchi kuwa kazi ya serikali ni kuwaletea maendeleo badala
yake wawahimize kufanya kazi na wajibu wa serikali ni kuwatengenezea
fursa iliwaweze kufanikiwa.
Kandege aliyasema hayo jana wakati
akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Rukwa ambapo alizungumza na watendaji
wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Alisema kuwa bado kunadhana kwa wananchi
kuwa kazi ya serikali ni kuwaletea maendeleo matokeo yake wamekuwa wakibweteka
katika kufanya kazi wakitegemea serikali itawaletea maendeleo wakati sera ya
serikali ya awamu ya tano inasisitiza kila mtu afanye kazi.
Aidha waziri Kandege aliwaonya
watumishi wa idara ya elimu mkoani humo kuacha kufanya matumizi mabaya katika
fedha za capitation kwani kumekuwepo na taarifa kuwa wamekuwa wakitumia fedha
hizo vibaya watambue serikali haiwezi kuvumilia kuona matumizi hayo
mabaya.
Awali alitoa akimkaribisha waziri
huyokatibu tawala msaidizi wa mkoa wa Rukwa anayeshughulikia tawala za mikoa na
Serikali za mitaa Albinus Mgonyani alimwambia kuwa mkoa huo unakabiliwa na deni
kiasi cha shilingi milioni 538 ambalo wakulima wanadai kupitia wakala wa
chakula wa taifa NFRA mkoani humo.
Alisema wamekwisha fanya mchakato
ili liweze kulipwa lakini pia alimuomba waziri huyo awasaidie kulisukuma ili
lilipwe haraka kwani wakulima wanazihitaji fedha hizo ziwasaidie kununua
pembejeo za kilimo katika msimu huu ambao tayari umekwisha anza.
Post a Comment