TANZIA SHABKI WA YANGA AMEKUFA
Taarifa za awali zinasema shabiki huyo amefikwa na umauti katika kijiji cha Chipogolo kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma njia ya kwenda mkoani Iringa kilichosababishwa na ajali ya gari.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake amesema marehemu alikuwa na wenzake watatu kwenye gari aina ya Rav 4 iliyopinduka kabla ya shabiki huyo kurushwa nje ya gari.
Kutokana na kurushwa kwake nje ya gari hilo dogo imeelezwa kuwa ndiko kilichopelekea kifo chake kwani wenzake wawili wamejeruhiwa pekee akiwemo dereva wa gari hilo.
Ally Yanga alikuwa kwenye majukumu rasmi ya kukimbiza mwenge wa uhuru akiwa kama muhamasishaji kwenye mbio hizo zinazoendelea nchini ambazo kwa sasa zipo mkoani Dodoma.
Post a Comment