WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA ILEJE BAADA YA KUMSHAWISHI MTOTO ASIENDELEE NA MASOMO
Joyance Kibona(59)na Eras minga(33) Wote wakazi wa
kijiji cha Ilondo wilayani ileje mkoani Songwe wamepandishwa kizimbani katika
mahakama ya wilaya ya ileje mkoani hapa kujibu shitaka la kula njama
kumshawishi mwanafunzi kuto endelea na masomo kinyume na kifungu cha sheria
namba 149 sura ya 16 kanuni ya adhabu .
Akisoma maelezo ya awali mwendesha
mashitaka wa polisi mahakamani hapo Charles Paulo amesema washitakiwa wote kwa
pamoja ambao ni wanandoa walitenda kosa
hilo Agost 25 mwaka huu walimshawishi mtoto wao ktoendelea na masomo wakijuwa
ni kinyume na taratibu za nchi.
Paulo amesema mwanafunzi huyo alikuwa
mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Namasele kata ya Malangali
wilayani hapa na alitarajia kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba katika
mtihani uliofanyika mwaka huu.
washitakiwa hao wamekana kutenda kosa
linalo wakabili na hakimu anayesikiliza kesi hiyo mahakamani hapo Charles
Christopher Makwaya ameahirisha kesi hilo mpaka itakapotajwa tena desember 9
mwaka huu kwajiri ya kusikiliza utetezi upande wa mashitaka.
Post a Comment