CCM WAAHIDI KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA HICHO KWA KULETA MAENDELEO
Mbeya
UONGOZI mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Wilayani Kyela mkoani Mbeya umejipanga kuisimamia serikali katika utekelezaji
wa Ilani ya Chama hicho katika kuwatumika wananchi katika kuondoa kero sugu na
kuwaletea maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa jana na katibu
wa Itikadi siasa na uenezi wilayani humo Emmanuel Mwamulinge katika kikao
cha kamati ya siasa ya wilaya ikiwa ni kikao cha kwanza baada ya kuchaguliwa
ambapo walipanga mikakati mbalimbali ya kukiimarisha cham hicho na kuwatumikia
wananchi.
Amesema uongozi huo mpya kwa
kushirikiana na madiwani,Mbunge na mkuu wa wilaya utahakikisha unasimamia
huduma za jamii zinazotekelezwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
wanaondoka kero ya muda mrefu ya ukosefu wa dirisha maalum kwa wazee na
watoto wanaotakiwa kutibiwa bure.
Aidha amelisema chama cha mapinduzi
wilayani humo kwa sasa kimejipanga kuhakikisha migogoro ndani ya chama hicho
haipati nafasi kwani wao kazi kubwa waliyonayo ni kuhakikisha
wanashikamana kusimamia ilani na sio kutumia muda mwingi kusuluhisha migogoro
isiyokuwa na tija.
Pia ameongeza kuwa wanaweka
utaratibu wa kukutana na wale ambao waligombea nafasi mbalimbali katika
chama hicho na kura zao hazikutosha kuwapa ushindi kushirikiana nao
katika mambo yanayohusu chama hicho.
Awali chama cha mapinduzi wilayani
kyela kilikumbwa na migogoro iliyopelekea baadhi ya madiwani kususia vikao vya
baraza wakimtuhumu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Dk Hunter Mwakifuna kuwatetea
baadhi ya watendaji waliokuwa na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma.
Mgogoro huo uliuodumu kwa zaidi ya
miezi 13 ulipelekea makamu mwenyekiti wa CCM taifa na Mwenyekiti wa kamati ya
maadili wa chama hicho Phillipo Mangula kufika wilayani humo kutatua mgogoro
ambao hata hivyo ulishindikana na hivyo mgogoro huo kumalizwa na waziri mkuu
Kassim Majaliwa.
Post a Comment