MKUU WA MKOA RUKWA ZELOTE STEPHEN AAGIZA KILA HALMASHAURI KUWA NA MAGULIO RASIMI YA UUZAJI MAHINDI
RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote
Stephen ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapa kuhakikisha wanakuwa na magulio
rasmi ya kuuzia mahindi ili wakulima na wafanyabiashara waweze kufuata
utaratibu.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa na
usimamizi thabiti na taratibu za uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za
jirani utafuatwa pamoja na mamlaka husika kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa
sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na halmashauri kupata mapato na nchi kwa
ujumla.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya
ghafla katika Kijiji cha Safu, kilichopo mpakani mwanchi ya Tanzania na Zambia na kujionea malori yenye
shehena za mahindi yakiingizwa kiholela kutoka katika nchi ya Zambia bila ya
kuwepo kwa mamlaka husika zinazosimamia uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi
za jirani.
Na kuongeza kuwa hakuna tatizo kufanya biashara na nchi za jirani isipokuwa biashara hizo zifanywe kihalali kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Halikadhalika Mh. Zelote Amesema kuwa Mkoa wa
Rukwa una mahindi ya kutosha na wafanyabiashara wa mikoa mingine wafike kununua
na sio kuvuka mipaka kwa njia za kupanya kufanya biashara hiyo.
Wafanya
biashara kwa upande
wao wamekaidi kuwa mahindi
yanayotoka Zambia bei yake ni nafuu zaidi kuliko ya Tanzania lakini pia
wakulima wa Tanzania huficha mahindi yao wakisubiri kupanda kwa bei jambo
ambalo ni hasara kwa wafanyabiashara wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa.
Post a Comment