WATOA ELIMU KWA WATOTO WA SHULE ZA AWALI NAMNA YA KUVUSHANA BARABARANI
Songwe
Shirika
lisilo la kiserikali la Save the Children chini ya meneja wa mradi,Elimu
Kayange,wameendesha mafunzo kwa wanafunzi wa shule 13 zilizopo mkoani songwe jinsi
ya kuvushana barabarani,kwani kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto wameamua
kuendesha mafunzo ili kunusuru vifo vya watoto wasiokuwa na hatia.
Shirika hilo tayari limetoa mafunzo
kwa shule zilizopo barabara kuu ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga,Mbozi
kwenda Ileja na Vwawa kwenda Mbeya na kwamba mkakati wa shirika ni kuzifikia
shule 100 huku akipongeza ushirikiano mzuri wa walimu na wazazi wanaoupata.
Hatua hiyo imekuja baada ya kiripotiwa
kwa matukio kadhaa ya baadhi ya wananfunzi wanaosoma katika shule zilizopo
pembezoni mwa barabara mkoani Songwe kugongwa na vyombo vya moto akiwemo mwanafunzi wa
darasa la awali Ratifa Masoud kugongwa na pikipiki wakati akivuka barabara..
Baadhi ya walimu ambao wamekuwa
wahanga wa wanafunzi wao kupata ajali za kugongwa na vyombo vya moto Abron
Popele na Meeda Mwakalinga wamesema ni zaidi ya miaka mitano wanafunzi wamekuwa
wakipata majeraha kwa sababu ya kugongwa na vyombo vya moto hasa pikipiki,na
kwamba wamepeleka taarifa hizo halmashauri ya wilaya ya Mbozi ili kudhibiti
hilo ikiwa ni pamoja na kuweka matuta pamoja na alama za barabarani .
Kwa upande wake wakala wa barabara
mkoani Songwe injinia Robat Nyengo akizungumza kwaniaba ya meneja wa mkoa,licha
ya kukiri kuwepo na ajari hizo,amesema tayari wamepata mkandarasi ambapo ndani
ya siku 14 atakamirisha uwekaji wa alama hizo.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo
licha ya kulipongeza shirika hilo,amesema kwa kutoa mafunzo hayo,anauhakika
wanafunzi watakuwa salama wakati wa kuvuka na kwamba kuhusu wanafunzi kugongwa
atazungumza na meneja wa wakala wa barabara (Tanroad) mkoani Songwe,ili waweze
kuweka alama za pundamilia na matuta maeneo yote hatarishi ili kuondoa hatari
ya wanafunzi kugongwa.
Post a Comment