OPERESHENI YA KUWAKAMATA WANAOJIHUSISHA KIMAPENZI NA WANAFUNZI YAANZISHWA MAKETE WAHUSIKA KUBURUZWA MAHAKAMANI
NJOMBE-MAKETE
Halmashauri
ya wilaya ya Makete imetangaza kiama kwa wazazi/walezi wa wanafunzi watoro
pamoja na wanaume waliowapa mimba wanafunzi na wale wenye mahusiano ya
kimapenzi na wanafunzi.Pia
imesema msako huo utawapeleka wahusika mahakamani na operesheni hiyo
itaendeshwa wilaya nzima
Katika taarifa iliyotolewa na mwanasheria wa wilaya ya Makete Godfrey Gogadi kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ilisema kuwa
kuanzia tarehe 28/10/2017 itafanyika operesheni wilaya nzima ya kukamata na
kuwafikisha mahakamani wazazi au walezi wote wenye wanafunzi watoro na watu
wote wanaojihusisha kimapenzi na wafunzi.
‘’hivyo basi wazazi au walezi wote wanatakiwa
kuhakikisha kuwa watoto au mtoto wako yupo shuleni kuanzia tarehe 23/10/2017’’ilisema
taarifa hivyo nakuongeza’’kila mzazi au
mlezi mwenye mwanafunzi mtoro au an amimba afike shuleni Tarehe 23/10/2017
akiwa na mtoto wake na kuonana na mkuu wa shule kwaajili ya kuripoti na kupata
maelekezo’’
Aidha
kupitia taarifa hivyo imeelezwa kuwa wazazi
ambao watakuwa hawajaripoti shuleni wakiwa na watoto wao amabo
wameathirika na utoro au mimba watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo
kufikishwa mahakamani na watatafutwa popote pale atakapokuwepo nchini au nje ya nchi.
‘’wananchi
na wazazi mnakumbushwa kuwa ni wajibu nwenu kisheria kuhakikisha wanafunzi
wanafika shuleni bila kukosa na hawapati
mimba wakiwa shuleni au nyumbani na kufuatilia maendeleo ya kila siku’’ilisema sehemu
nyingine ya taarifa hiyo.
Katika
hatua nyingine wakuu wa shule,walimu wakuu na walimu wote wametakiwa kuandaa taarifa ya wanafunzi
watoro na wenye mimba na kuifikisha taarifa hiyo kwa viongozi wa vijiji na
kata.
Pia
wameagizwa kuhakikisha majina ya watu
wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi yanakuwepo kwenye ofisi za kata na
kufikishwa vituo vya polisi wilayani humo.
Takwimu
zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi August mwaka 2017 mkoa wa Njombe ulikuwa na
jumla ya wanafunzi 62 wenye mimba katika shule
za msingi na sekondari huku kati ya hao wanafunzi 53 ni wa sekondari na
wanafunzi 9 ni wa shule za msingi.
Post a Comment