MADIWANI WILAYANI KALAMBO WAITAKA SERIKALI KASAMBAZA HUDUMA ZA MAJI VIJIJINI
Madiwani wilayani kalambo wakiwa katika moja ya vikao vyao |
RUKWA-KALAMBO
MADIWANI
katika wilaya ya kalambo mkoani Rukwa
wameiomba serikali kusambaza huduma
ya maji kwenye kata na vijiji tofauti
wilayani humo ili kuwasaidia wananchi
hususani akina mama kuondokana na adha ya
kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta
huduma hiyo muhimu.
Wakiongea
na kituo hiki wakati wa kikao cha
baraza la madiwani wilayani humo , madiwani
hao wamesema wananchi wamekuwa wakilazimika
kutembea umbali mrefu wakati wa
kutafuta huduma ya maji na
huku kwa baadhi ya maeneo wakiuziwa
maji kwa bei kubwa na kupelekea kujitokeza
kwa mara ramiko yasio kuwa na ukomo.
Wamesema
licha ya hilo serikali haina
budi kuchimba visima kwenye zahanati na
vituo vya afya ili kuwapunguzia
adha hiyo wananchi ambao hufika
kwenye vituo hivyo kwa lengo la
kupata matibabu.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Daudi Schone , ambae
mbali na kuli kuwepo adha hiyo
amesema serikali inategemea kufufua
miradi yote ya maji ya
yazamani sambamba na kuunda kamati maalumu
ambayo itasaidia kusimamia miradi hiyo ili
ikamilike kwa wakati.
Post a Comment