MKUU WA MKOA WA RUKWA KAMISHNA MSTAAFU ZELOTE STEPHEN AMEWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI YA SUMBAWANGA VIJIJI NA MANISPAA KUHAKIKISHA WANAMALIZIA UJENZI WA BARABARA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnamStaafu Zelote Stephen amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga vijiji na Manispaa kuhakikisha wanamalizia ujenzi wa barabara ya Mollo - Songambele Azimio kabala ya Msimu wa Mvua kuanza. |
Ametoa agizo hilo
baada ya kutembelea katika kijiji hicho kuona maendeleo ya miti aliyoshiriki
kuipanda pamoja na wanakijiji hao katika maadhimisho ya siku ya kupanda miti
kimkoa tarehe 19/1/2017 ambapo siku hiyo aliahidi kuwajengea barabara hiyo.
"Wakurugenzi
nataka kabla ya Mvua kunyesha barabara hiyo iwe tayari, Mkurugenzi wa
Sumbawanga Vijiji kwakuwa wewe umesema kipande chako ni kidogo sana basi
ukimaliza kesho nitafurahi sana." Alisema.
Nao kwa upande wao
kila mmoja baada ya kupewa nafasi Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Suumbawanga
Saad Mtambule alisema kuwa barabara hiyo imeshaanza matengenezo kwa kiwango cha
changarawe na kuwa inaendelea vizuri.
Nae Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini Nyangi Msema Kweli aliahidi kuwa ahizo hilo
litatekelezwa kwani tangu ahadi itolewe mwanzoni mwa mwaka huu, halmashauri
ilishaiweka barabara hiyo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 na
kuwaahidi kuwa pesa ipo ya kufanaya matengenezo hayo.
msisitizo huo uliibuka
baada ya Diwani wa Msanda muungano Mh. Charles Kanoni kuanza kufanya
mikutano na kuwaambia wananchi kuwa barabara hiyo haitatengenezwa kakuwa
haikuwa kwenye bajeti yoyote ya halmashauri ya Sumbawanga Vijijini jambo ambalo
lilimshtua Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule.
Dk. Haule alisisitiza
kuwa alitegemea diwani kuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo na badala
yake anakuwa kinyume na matarajio ya wanakijiji na kumuonya kutojihusisha na
kusema uongo kwa wananchi ili ajitengenezee ulaji na kuongeza kuwa serikali ya
awamu hii inatekeleza ahadi zake zote na hakuna ahadi itakayotolewa ambayo
haitatekelezwa.
Ziara hiyo ilikuwa
maalum kwaajili ya kuhamasisha upandaji wa miti katika kijiji hicho ili kiwe
cha mfano katika Wilaya na Mkoa wa Ujumla juu ya upandaji wa Miti.
Aidha, Mh. Zelote pia
aliahidi kukisaidia kikundi cha ngoma cha Mwalimu Nyerere cha kijiji hicho
kuimarisha vifaa vyao na hatimae kuendelea kufanya shughuli zao kwa ufanisi na
kujiongezea kipato katika shughuli zao za kila siku.
"Kama nilivyoahidi
nilipokuja mwanzoni mwa mwaka huu leo hii nimetoa shilingi 167000 kwa kikundi
hiki ili waboreshe vifaa vyao vya kazi," RC alisema.
Na kuwaomba wadau
mbalimbali wa utamaduni kujitokeza kusaidia kuuinua utamaduni wa wafipa na wa
mkoa kwa ujumla.
Post a Comment