JESHI LA POLISI MKOANI MMBEYA LASHIKILIA WATU WANNE KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI
MBEYA
JESHI la polisi mkoani Mbeya
limewakamata watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi kwa tuhuma za kuteka basi
kisha kupora simu na fedha.
Akizungunza jana na gazeti hili
kamanda wa polisi mkoani Mbeya Mohammed Mpinga,alisema tukio la kutekwa basi
lilitokea siku ya tarehe 28 agosti mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika
kitongoji cha Logia kijiji na kata ya Upendo wilayani Chunya mkoani hapa.
Kamanda Mpinga alisema baada ya
tukio hilo la utekaji wa basi uliofanywa na watu hao,wamefanikiwa kupora fedha
Milioni 2.2 pamoja na Simu zenye thamani ya laki 4,10,000.ambapo basi
lilnalofanya safari yake kutoka Chunya kwenda Mbeya lilitekwa na wavamizi hao
ambao wamefanikiwa kupora vitu hivyo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Juakali
Mbaramwezi,Gosper Mahini,wakazi wa Sumbawanga na Petrol Juma na Andrew Herman
wakazi wa Chunya,ambapo kamanda Mpinga alisema kuwa jeshi lake linaendelea
kuwasaka waharifu wawili waliosalia baada ya kupata taarifa kuwa waliohusika na
utekaji huo walikuwa sita.
Alisema katika utekaji huo,hakuna
mtu yeyote aliyefariki wala kupotea baada ya kuwepo kwa taarifa za uvumi kuwa
kuna watoto wawili walitekwa na kwamba watu hao waliteka gari zima kisha
kuchukua fedha na simu na kuamua kutokoma licha ya kuwa jeshi limewakamata.
Mponga,aliwasa wananchi kutoa
ushirikiano na jeshi la polisi kuwafichua waharifu na kwamba hata vitendo vya
watu kujichukulia sheria mkononi.
''Jeshi lapolisi litawakamata hao
waliosalia kwa kuwa hakunaanayeweza kupingana au kukwepa mkono wa sheria na
kwmba endapo kutakuwa na dariri za watu hao kujifichanmahali furani wananchi
wanatakiwa kutoa taarifa polisi,eneo hilo ambalo watu wanatekwa jeshi
litahakikisha linaweka ulinzi thabiti''alisema kamanda Mpinga.
Post a Comment