MKOA WA SONGWE WASHIKA NAFASI YA PILI KUTOKA MWISHO KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
MBOZI-SONGWE
IMEELEZWA kuwa Mkoa wa Songwe
umeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika mikoa yote nchini kwa uchafuzi wa
mazingira huku mkoa wa Mara ukishika nafasi ya mwisho,hali iliyozua taharuki
kwa mkuu wa mkoa huo mbaye amepanga mikakati ili kuondokana na kushika nafasi
hiyo ya mwisho.
Kauli hiyo imetolewa leo (jana) na
mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa,kwenye kikao cha pomoja na viongozi wa
serikali kutoka wilaya zote za mkoa huo huku akieleza kusikitishwa kwake mkoa
huo kushika nafasi ya pili kutoka mwisho.
''Nasikitika sana kuona takwimu
imetolewa kuwa Songwe ni ya pili kutoka mwisho,kwa usafi wa mazingira,kwa hali
hiyo nataka maafisa wa afya kuhakikisha wanasimamia hali ya usafi wa mazingira
ili kuondokana na hali ya kushika nafasi hiyo.
George Mgalla Afya mkoani
Songwe,alisema kila halmashauri ilipata Milioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa
shughuri za usafi wa mazingira Ambapo mkoani yaani Songwe ilipewa Milioni 10
ambapo utekelezwaji umefanyika licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Alisema changamoto inayowakumba ili
kushindwa kufikia lengo hilo, ni upungufu wa watumishi wa idara ya afya,ufinyu
wa bajeti,maafisa afya kutosimamia sheria zilizopo za mazingira,kutofanyika kwa
ukaguzi wa wa mara kwa mara wa mazingira kwenye kaya na kwamba ili kufanikisha
hilo,changamoto hizo zitatuliwe.
Kufuatia hali hivyo, Galawa alitoa
agizo kwa maafisa wa idara ya afya kuhakikisha wanafanya ziara maeneo yote na
kuhakikisha inawachukulia hatua wananchi ambao watashindwa kujenga vyoo bora
ikiwemo kuwapeleka mahakamani.
Alisema halmashauri zote zihakikishe
zinatumia sheria zilizopo na kutunga sheria ndogo ndogo za kuwabana wananchi
wanaokaidi agizo la serikali la utunzaji wa mazingira ikiwemo kuhakikisha kila
kaya inakuwa na choo bora kuliko ilivyo hivi sasa ambapo taka zinazagaa
ovyo,baadhi ya shule hazina vyoo hii haikubariki.
Hata hivyo Galawa alitoa siku 30 kwa
wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya zote kuhakikisha zinaondoa tatizo
la ukosefu wa vyoo kwenye kaya na uchafuzi wa mazingira na kuhakikisha wanaweka
utaratibu wa kuyakagua magari yote yatakayokosa chombo cha kutunzia taka.
Post a Comment