SHULE YA MSINGI MANGA MKOANI SONGWE INA UPUNGUFU MKUBWA WA MADARASA.
TUNDUMA-SONGWE
SHULE ya msingi Manga iliyopo
halmashauri ya mji wa Tunduma mkoani Songwe,inakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa huku ikiwa na idadi ya wanafunzi zaidi ya
3,000 ambapo vyumba 70 vinahitajika kulingana na uwingi wa wanafunzi ambapo
vyumba vilivyopo ni 8 pekee.
Shule ya msingi Manka,ni mpya
imejengwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzikatika shule ya msingi
Tunduma,lakini hali ya shule hiyo ni mbaya kutokana na kuwepo kwa wanafunzi
3139 wanaotumia vyumba vya madarasa 8 kati ya 70 vinavyohitajika.
Baraka Osiah ni mwanafunzi shuleni
hapo,alisema katika dawati moja wanalazimika kukaa wanne hadi watano kutokana
na uwingi wao huku miundombinu ya shule hiyo ikiwemo ukosefu wa sakafu ikiwa ni
moja ya kikwazo cha wao kusoma kwa manufaa.
Yassin Mussa mkuu wa shule
hiyo,amekiri wazi kuwepo kwa changamoto hizo na kusema kuwa idadi ya wanafunzi
hao 3139 nikubwa ukilinganisha na vyumba 8 vya madarasa vilivyopo huku kukiwa
na mahitaji makubwa ya walimu na kwamba ili kuondokana na hali hiyo,wanaomba
serikali na wadau kuisaidia shule hiyo,
Kufuatia changamoto hiyo,meneja wa
Benk ya Posta Tanzania Regina Semakafu alimkabidhi mkuu wa wilaya ya Momba
mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya shilingi Milioni 1.5,kwa ajili ya
kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa,na kuahidi kuendelea kuchangia pale
itakapo hitajika.
Akipokea msaada huo,mkuu wa wilaya
hiyo,Juma Irando licha ya kuipongeza Benki kuwapatia saruji,alisema itatumika
kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali zenye
uhitaji ikiwemo shule hiyo ya Manga yenye upungufu mkubwa.
Alisema kutokana na changamoto
zilizopo za uhaba wa vyumba vya madarasa alitumia nafasi hiyo,kuwaomba wadau
wengine kusaidia kuondoa changamoto hiyo kwa kuwa elimum ndiyo msingi thabiti
wa maengeleo kwa mustakabari wa maisha ya sasa.
Post a Comment