WANANCHI MKOANI SONGWE WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANATOA TAARIFA SAHIHI ZA UKAZI NA UTAIFA KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI VITAMBILISHO
SONGWE
KATIBU
tawala mkoani Songwe,Herman Tesha amewataka wananchi katika wilaya zote
za mkoa wa Songwe,kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi ukazi na utaifa
kwenye zoezi la uandikishaji wa vitambirisho vya utaifa linaloratibiwa
na wakala wa vitamburisho nchini NIDA huku akiwataka viongozi wa
serikali za vijiji kutoa ushirikiano ili kuhepuka taarifa za udanganyifu
kwenye rekodi hizo.
Akizungumza
na gazeti hili,katibu Tesha,alisema Songwe ni moja ya mikoa iliyopo
kwenye maeneo ya mipaka hivyo akasisitiza umakini mkubwa katika zoezi
hilo,la uandikishaji akiwataka viongozi wa serikali za mitaa na vijiji
pamoja na vyombo vya dora kuhakikisha hakuna udanganyifu katika
kukusanya taarifa sahihi za watu wanaosajiliwa hasa katika makundi ya
wakimbizi na uhamiaji.
Colletha
Peter,Afisa usajili wa vitamburisho mkoani Songwe,alisema uandikishaji
vitamburisho vya Taifa umeanza kufanyika takribani mwezi mmoja sasa na
kusema kuwa tayari wananchi 98628 wamesajiliwa na kupatiwa vitamburisho
huku muitikiao ukionekana kuwa mzuri.
Msimamizi
wa kampeni za uandikishaji Magreth Gabriel aliwataka wananchi kuendelea
kujitokeza kwa wingi ili kila mwananchi ajipatie kitamburisho n akwamba
zoezi hilo bado linaendelea huku akijiapiza kufanya kazi kwa uadirifa
kwa kufuata kanuni na sheria za nchi zilizowekwa.
Eliza
Amanyisye mkazi wa Songwe,alisema kutokana na umuhimu wa kupata
vitamburisho hivyo,wao kama wananchi katika maeneo yao,wamekuwa
wakihamasishana kwenda kujiandikisha ambapo alisema muitikoa ni mzuri.
Anna
Mlawa,mkazi wa Songwe,alisema zoezi linaendelea vizuri kwani wananchi
wengi wanajitokeza kujiandikisha pia akatoa rai kwa serikali kuwa makini
na watu wanaotoka nje ya nchi hasa kwa mkoa wao ambao unapakana na nchi
nyingi ikiwemo,Zanbia,Malawi na Congo ili isije kuonekana watu wa nchi
hizo wamejiandikisha kinyemela na kuonekana ni raia wa Tanzania.
Hata
hivyo,msimamizi wa NIDA nyanda za juu kusini Fransisi Saliboko alisema
zoezi hilo linalenga watu wa makundi matatu ambao ni
Watanzania,wahamiaji walowezi na wakimbizi,na kwamba zoezi hilo
litaendelea kufanyika kwa kufuata misingi iliyowekwa na jamhuri ya
muungano wa Tanzania kwa afya ya watanzania wote.
Post a Comment