WANANCHI WA KATA YA IVUNA WILAYA YA MOMBA MKOANI SONGWE WAMEJITOLEA KUJENGA KIWANDA CHA CHUMVI
MOMBA-SONGWE
WANANCHI wa vijiji vya Itumbula na Ivuna kata ya Ivuna wilaya ya Momba mkoani Songwe wameungana na kujenga Mradi wa kuzarisha chumvi kwenye bwawa la maji ya chumvi.
Aidha imedaiwa kuwa mradi huo utakapokamilika utanufaisha nchi nzima na kuongeza ushindani katika soko la chumvi ndani na nje ya nchi na kwamba kiwanda hicho kilitelekezwa miaka sita iliyopita ambapo kilizalisha chumvi yenye ubora wa daraja la 3 kitaifa
Wananchi hao wamesema wameamua kujitolea kujenga mradi hu, huku serikali ikiwaunga mkono wananchi hao kuhakikisha kiwanda kinakamilika na kusema kuwa awali miaka sita iliyopita kiwanda hicho kabla ya kutelekezwa kilizalisha chumvi hiyo iliyoshika nafasi ya 3 kitaifa kwa ubora.
Viongozi wa kijiji na kata kwa pamoja wameiomba serikali iwasaidie kupata wawekezaji ili watakapoanza usarishaji waweze kuwa na uhakika wa kuzalishaji chumvi iliyo bora nay a ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya momba Adrian Jungu amekiri kuanza ujenzi wa mradi na kwamba halmashauri imewaongezea wananchi sh. Mill 50 ili kukamilisha mradi huku akieleza namna ya upatikanaje wa soko la uhakika.
Post a Comment