AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA KWA UTAPELI
KATAVI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa
wa Katavi imemuhukumu Kapele Mpundililwa(36)mkazi wa Namanyere
wilayani Nkasi mkoani Rukwa kutumikia kifungo
cha miaka mitatu jela baada ya kumtia hatiani kwa utapeli
na kujipatia fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni
3.9
Mtuhumiwa huyo alijipatia fedha hizo baada ya kuwalagai
vijana 144 kuwa atawapatia ajira katika Taasisi iIsiyo ya kiserikali ya
APAPO.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu
mkazi wa mahakama ya mkoa wa Katavi
Odira Amworo baada ya kuridhika pasipo shaka yoyote na
ushahidi uliotolewa.
Awali katika
kesi hiyo mwendesha mashta mwanasheria
wa Serikali wa mkoa
wa Katavi Peter Maiko alidai
mahakamani hapo kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo mei 23, 2013 wilayani Mpanda
kwa nyakati tofauti.
Mwanassheria huyo alidai kuwa
mshitakiwa Kapeele alifika wilayani
Mpanda na kujitambulisha kuwa ni Mkurugenzi
ya Asiasi ya Shirika la Umoja wa Watu
wa Afrika APAPO na alianza kutangaza nafasi
mbalimbali za ajira kwaajiri .
Miongoni mwa njia
alizotumia kujipatia fedha baada ya kutangaza ajira
alimtaka kila aliyeomba atoe kiasi cha fedha iliapate kazi.
Mwanasheria Peter Maiko aliieleza
mahakama hiyo kuwa ajira kwa ngazi ya mtaa na
wilaya kiwango cha ada ya maombi
ya ajira kilikuwa ni shilingi 17,000
na sifa ilikuwa mwombaji lazima
awe na elimu ya darasa la saba hadi
kidato cha nne na ajira kwa ngazi
ya mkoa ada ilikuwa ni shilingi
160,000 na anaeomba ajira awe
na sifa ya kuanzia stashahada.
Alidai
kuwa mshitakiwa huyo katika
utapeli huo alifanikiwa kuwadanganya watu 144 ambao
walilipa ada za maombi
ya ajira hizo na kujipatia kiasi cha milioni 3,980,000
ambazo zote ziliingizwa
kwenye akaunti aliyokuwa amewapatia
na shughuli hiyo ya kutafuta watu
kwa ajiri
ya ajira alikuwa akifanya yeye pamoja na wasaidizi
wake wanne ambao walitoroka baada
ya mkurugenzi wao Kapeele kukamatwa
mkoani Kigoma baada ya kuwa ametoroka
mkoani Katavi.
Akisoma hukumu hiyo hakimu
Amwolo aliieleza
mahakama kuwa kutokana na mwenendo
mzima wa kesi hiyo
na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo na
upande wa mashitaka pasipo shaka yoyote imemtia
mshitakiwa hatiani.
Hakimu Amwolo alieleza
kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia hatiani mshitakiwa
ni hati za waliotapeliwa ajira walizolipia
benki ambazo zilipelekwa mahakamani
hapo huku zikiwa na majina ya waliotapeliwa
na kiasi cha fedha walizoingiza kwenye akaunti
ya mshitakiwa
Alisema mshitakiwa amepatikana na hatia
ya kifungu cha sheria namba 302
cha kanuni ya adhabu sura ya
16 ya marekebisho ya mwaka 2002
hivyo Mahakama
imemuhukumu mshitakiwa kutumikia jela kifungo
cha miaka mitatu kuanzia jana.
Mwisho
Post a Comment