MKUU WA MKOA WA RUKWA WANGABO AAGIZA KUKAMATWA KWA WAZAZI NA WANAFUNZI WA KIKE WATAKAOBAINIKA KUWA NA UJAUZITO
Rukwa
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakuu wa shule
Mkoani humo kumkamata na kuwaweka ndani wazazi na mwanafunzi yeyote wa kike
atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja aliyesababisha mimba hiyo.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia ya kumalizana
kienyeji huko majumbani na matokea yake watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika
ili waweze uwajibishwa na hatimae kupunguza kasi hiyo ya mimba kwa wananfunzi.
Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa
ya shule ya sekondari Kirando, Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua
ujenzi wa maabara wa shule hiyo pamoja na na kuongea na wanafunzi, taarifa
iliyobainisha kupatikana kwa mimba saba kwa kipindi cha Januari hadi oktoba
mwaka huu na kesi zote zipo polisi.
Halikadhalika ametahadharisha kuwa shule
yeyote atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika
Halmashauri nne za mkoa huo, ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa
watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi
hizo polisi.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Kirando Erneo Mgina amesema kuwa kati ya wanafunzi saba waliopata
ujauzito wanafunzi watatu ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O – Level” na
kueleza kuwa wengi wao hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini pale tu
wanaporudi shule na kuwapima.
Post a Comment