MKUU WA WILAYA YA ILEJE JOSEPH MKUDE AAGIZA KUCHUKILIWA HATUA ZA KISHERIA WATENDAJI WANNE
Ileje
Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani
Songwe Joseph Mkude amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Ileje mkoani hapa Haji Mnasi kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wa 4
ambao wamebainika kufanya kazi pasipo kufuata taratibu za kitumishi wilayani
hapa.
Mkude ametoa agizo hilo hivi
karibuni katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi
uliopo katika ofisi za boma ambapo amesema mtumishi wa serikali kufanya kazi
kwa matakwa yake katika kituo cha kazi ni utovu wa nidhamu.
Aidha mkuu huyo amesema serikali
haitawavumilia watendaji ambao hawawajibiki katika vituo vya kazi hali ambayo
itapelekea kukwamisha maendeleo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuzorotesha
vyanzo vya mapato katika maeneo husika husika.
Mkrugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya wilayani hapa Haji Mnasi amesema watendao ambao wamewajibishwa ni pamoja
na walinzi wawili wa kwenye mageti,mtendaji wa kijiji mmoja na wa kata mmoja
hali ambayo amesema hawatawavumilia watendaji wazembe kazini.
Post a Comment