Header Ads


Wafugaji Momba wapata hofu juu ya Mifugo yao

Momba-Songwe
WANANCHI jamii ya wafugaji,katika halmashauri ya wilaya ya Momba mkoani Songwe,wamekumbwa na hofu baada ya mbuzi zao kufa wakiwa zizizni kwa kukumbwa na ugonjwa wa mapafu huku wakiwatuma madiwani wao kueleza kikao cha baraza ili mbuzi wao wapatiwe chanjo kuondoa vifo vilivyopo.
Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha wazi cha baraza la madiwani kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri mjini Chitete ambapo madiwani waliiomba halmashauri kuwaondolea hofu wafugaji katika kata zao kwa kuzipatia chanjo mbuzi hizo.
Correta Mwaselela diwani kata ya Mkomba,alisema tatizo la mbuzi kufa limekuwa ni kubwa ambapo alisema juzi walifika wafugaji 6 nyumbani kwake wakimueleza kuwa mbuzi wao wamekufa zizini na kwamba baada ya kufika eneo la tukio aliona mbuzi wengi wakiwa wamekufa.
Alisema baada ya hapo aliwasiliana na uongozi wa halmashauri ambapo leo katika kikao hicho madiwani wengine wameeleza tatizo hilo pia kuwepo katika kata zao na kwamba kutokana na ukubwa wa tatizo hilo,ipo haja serikali kupitia halmashauri idara ya mifugo,kufika vijijini na kuwapatia chanjo mbuzi hao.
Dr,Adolf Wilkelm,afisa mifugo na uvuvi wilayani humo,akizungumza kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji Adrian Jungu, kupitia kikao hicho,alikiri kuwepo na maafa ya mbuzi hao na kusema kuwa ofisi yake ilipokea taarifa za ugonjwa huo,na kusema kuwa umetokea kutokana na mabadiriko ya tabia ya hewa,hivyo ni lazima wapatiwe chanjo.
Aliongeza kuwa wamewasiliana na uongozi wa kituo cha utafiti mkoani Iringa ambao waliwajibu kuwa dawa bado hazijafika huku akiahidi kuwa endapo dawa zitafika wataenda kuzichukua ili wapate kuwatibu mbuzi walioathirika na kuwapa chanjo waliowazima ili wasiugue.
‘’Ndugu zangu madiwani,ni kweli ugonjwa huo upo,ila kituo cha tiba kanda ya kusini kipo Iringa,tumewasiliana nao wamesema dawa zikifika watatujurisha ili tuzifuate na kuzitibu mbuzi zote,na pia dawa hizo zinauzwa chupa 1 sh,30,000 hadi 40,000 na inatibu mbuzi 100’’alisema Dr,Wilkelm.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya mbuzi walioathirika ni kata za Ivuna,Mkomba na bonde lote la Kamsamba,hivyo alitoa rai kwa wafugaji na wakulima kuwa wahamasishane kuchukua hatua ili kupunguza maafa wakati wao wakisubiri dawa zifike kituo cha utafiti mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Mathew Chikoti,alisema kutokana na mbuzi hao kuugua homa ya mapafu,waliagiza idara husika kuwasiliana na kituo cha utafiti kilichopo Iringa ili kupata dawa za chanjo ambapo tayari wamaefanya mawasiliano na dawa zipo njiani zinakuja.

No comments

Powered by Blogger.