Header Ads


Baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Momba Mkoani Songwe Wapitisha Bajeti ya bilioni 20.5

Momba-Songwe 
MADIWANI katika halmashauri ya wilaya ya Momba mkoani Songwe,wamepitisha mapendekezo ya bajeti Bilioni 20.5 katika mawaka wa fedha 2018-19 huku baadhi yao wakiijadili kuwa haiwezi kuondoa changamoto zilizopo kutokana na halamashauri hiyo kuwa na changamoto nyingi kutokana na upya wake.
Nerasto Simbeye diwani kata ya Mpapa alisema mapendekezo ya bajeti hiyo endapo makusanyo ya fedha yatafanikiwa yataweza kupunguza changamoto zilizopo lakini sio kumaliza kwa kuwa fedha ni ndogo kuliko matatizo yaliyopo na kwamba serikali inatakiwa iwape kipaumbele ili wafanikishe malengo yao.
Nasibu Mkoma diwani viti maalum,alisema bajeti ya fedha hizo haitoshi kuendesha halmashauri hiyo, kuwa ni mpya na inachangamoto nyingi na inategemea serikali kuiendesha halmashauri hiyo hivyo ipo haja ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kujikwamua.
Awali akisoma makisio hayo mbele ya kikao cha baraza la madiwani na watendaji katika ukumbi wa halmashauri hiyo mjini Chitete,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Adrian Jungu,alisema kamati mbalimbali zimepitia na kuona kuwa Bilioni 20.5.itaweza kukusanywa kwa mwaka huu wa fedha.
Alisema kutokana na hali halisi ya halmashauri hiyo ni ngumu kukusanya fedha zaidi ya hizo hivyo,kamati husika zimepitia kila chanzo na kuona uwezekano wa kukusanya kiasi hicho,hivyo kamati ya uchumi na fedha imepitisha na hivi sasa wanapitisha kwenye kikao cha baraza la wazi kwa ajili ya utekelezaji.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Mathew Chikoti,alisema ni kweli makisio hayo ni madogo lakini wasingeweza kukisia pakubwa kutokana na halmashuuri hiyo,kuwa mpya hivyo vyanzo vyake ni duni na kwamba sio mwisho wa makisio kwani wataendelea kubuni vyanzo na kuviweka kwenye bajeti ijayo.
Halmashauri ya Momba ni mpya imemegwa kutoka wilaya ya Mbozi mwaka 2015 ikiwa na changamoto lukuki ikiwemo ukosefu wa barabara,maji safi,hospitali ya wilaya,vituo vya afya na nyinginezo huku serikali ikijipanga kutatua kero hizo kutokana na fedha inayopatikana

No comments

Powered by Blogger.