WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI WILAYANI UKEREWE
UKEREWE-MWANZA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe na kuuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha maji hayo yanatoka wakati wote na mradi huo unakuwa endelevu.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe na kuuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha maji hayo yanatoka wakati wote na mradi huo unakuwa endelevu.
Waziri
Mkuu alizindua mradi huo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati
akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Alisema
Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na
salama nchini.
Baada
ya kuzindua mradi huo, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi wa mji wa
Nansio kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Getrude
Mongella, ambapo alisema mradi aliouzindua katika kijiji cha Bwasa ni
sehemu ya mradi wa maji wa Kazilankanda utakaohudumia vijiji 13 vya
wilaya hiyo.
Alisema
mradi huo unagharimu shilingi bilioni saba na unatekelezwa katika
vijiji vya Muhula, Mahande, Namasabo, Namagondo, Kazilankanda, Malegea,
Igalla, Kigara, Lutare, Busunda, Bwasa, Buhima, Hamuyebe na utahudumia
wakazi 68,038 pindi utakapokamilika.
Mkataba
wa Mradi huo ulisainiwa Machi 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo
April, 2018, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 5.637 sawa na
asilimia 78.26 tayari zimeshatumika na mradi umekamilika kwa asilimia 92
na tayari baadhi vijiji vimeanza kupata maji.
Waziri
Mkuu alisema mkakati wa Serikali ni kuwahudumia wananchi kwa kutatua
kero zinazowakabili ikiwemo ya upatikanaji wa maji, ambapo imedhamiria
kuendelea kusambaza huduma hiyo hadi vijijini ili kuhakikisha vyote
vinapata maji.
Waziri
Mkuu alisema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya
kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita
400 kutoka kwenye makazi yao.
Waziri
Mkuu aliwaambia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati
mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia
wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo
kuliko kutafuta maji.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Bw.
Estomihn Chang’ah apange siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero
mbalimbali zinazowakabili wananchi hususani za ardhi na kushirikiana nao
katika kuzipatia ufumbuzi.
Pia
Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa wilaya leo saa 3.00 asubuhi akiwa
na watumishi wa Idara ya Ardhi akutane na wananchi wote wenye malalamiko
ya ardhi ili ashirikiane nao katika kuyapatia ufumbuzi. Alitoa agizo
hilo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wananchi yahusuyo masuala ya
ardhi yaliyowasilishwa kwake kupitia njia ya mabango.
Alisema
kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi
kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu wa
nchi.
Awali,
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Luhaga Mpina aliwaomba wananchi
hao kutunza rasilimali zilizopo ndani ya ziwa Victoria na kujiepusha na
uvuvi haramu kwa sababu unatishia uwepo wa samaki ndani ya ziwa hilo.
Waziri
huyo alisema iwapo vitendo vya uvuvi haramu vikiachwa bila ya kuzuiwa
kuna uwezekano mkubwa wa samaki kutoweka ndani ya ziwa hilo baada ya
miaka miwili. Alisema tayari Serikali inaendelea na operesheni ya
kupambana na uvuvi haramu.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.
Post a Comment