WAZIRI MKUU AGIZA SEKONDARI YA PIUS MSEKWA IPEWE GARI
UKEREWE-MWANZA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati awe amepeleka gari katika shule ya Sekondari ya bweni ya Pius Msekwa ifikapo Februari 25 mwaka huu.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati awe amepeleka gari katika shule ya Sekondari ya bweni ya Pius Msekwa ifikapo Februari 25 mwaka huu.
Amesema
shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 700 lazima iwe na chombo cha
usafiri kitakachotumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja
na dharura za kuwapeleka hospitali wanafunzi pale wanapougua.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati
alipotembelea shule hiyo na kuzindua madarasa na mabweni yaliyojengwa
kupitia mradi wa Mpango wa Elimu wa lipa kulingana na Matokeo (EP4R).
“Wakurugenzi
mnatakiwa kutambua shule hizi ni zenu, hivyo mnapaswa kuzihudumia.
Shule hii inawafunzi zaidi ya 700 na wanalala hapa hapa hivyo lazima
kuwe na gari la kuwahudumia wanafunzi hasa wakati wa dharura.”
Alisema
Serikali haiwezi kuiacha shule hiyo bila ya kuwa na chombo cha usafiri,
ambapo alimsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anatoa
kipaumbele kwa taasisi za umma ili ziweze kutekeleza majukumu yake
ipasavyo.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu aliwwagiza Wakurugenzi wote nchini kushirikiana na
uongozi wa shule mbalimbali za Serikali katika kutatua baadhi ya
changamoto zinazoikabili.
Miongoni
mwa changamoto hizo ni malipo ya watumishi wasaidizi wakiwemo wapishi,
walinzi na madereva, ambapo aliwataka wachukue jukumu la kuwalipa
watumishi hao badala ya kuacha ya kuwaachia Wakuu wa Shule.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu aliziagiza halmashauri zote nchini
kuhakikisha zinamalizia ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule zao
zilizobaki na Serikali itasambaza vifaa vya maabara mara
zitakapokamilika.
Waziri
Mkuu alisema tayari Serikali ilishasambaza vifaa vya maabara katika
shule 1,696 za sekondari nchini ambazo zilikamilisha ujenzi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.
Post a Comment