Header Ads


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA NEC




 
 
 
 
 
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

 

                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inapenda kuutangazia umma kuwa upigaji kura   katika uchaguzi mdogo wa majimbo ya Kinondoni na Siha na   Kata nane umefanyika kwa Amani na Usalama

Hadi vituo vinafungwa, NEC haikupokea taarifa yoyote ya kuwepo  kwa matukio ya uvunjifu wa Amani. Kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza zilitatuliwa na wasimamizi wa uchaguzi jambo ambalo lilifanya uchaguzi katika maeneo yote ufanyike katika hali ya Amani.

 Hata hivyo kuna taarifa ambazo NEC imezipata kupitia vyombo vya habari kuwa katika kituo cha Idrisa, Magomeni  jimbo la Kinondoni,  kuna mtu alichukuwa sanduku la kupigia kura na baadaye kulirudisha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inafuatilia tukio hili na itutalitafutia ufumbuzi. Hata hivyo Tume imevishauri vyama vya siasa kufuata utaratibu wa kisheria kuwasilisisha malalamiko ndani ya chumba cha kupigia kura kwa wakala wa chama  kujaza fomu namba 14 kuhusu maandalizi ya kituo cha Kupigia kura kama anaridhika nayo ama la.

No comments

Powered by Blogger.